Habari za Punde

Kamati ya Muda ya ZFA Yakabidhi Vifaa vya Michezo kwa Timu za Mafunzo na JKU Iweze Kushiriki Vizuri Michuano ya Kimataifa.

Baadhi ya Mipira iliotolewa na CAF kwa Chama cha Mpira Zanzibar ZFA jumla ya mipira 100 imekabidhiwa kwa Chama hicho kwa ajili ya Timu zinmazoshiriki Michuano ilioandilwa na CAF na kwa matumizi ya Timu ya Taifa ya Zanzibar na kuchuano inayoandaliwa na CAF. timu ya Mafunzo na JKU zimekabidhiwa mipira 10 kila noja kwa ajili na kujiandaa ni michuano ya CAF kwa timu hizi zinazoiwakilisha Zanzibar mwezi ujao.
Katibu wa Kamati ya ZFA Hashim Salum, akizungumza na waandishi wa habari za michezo Zanzibar wakati wa hafla ya kukabidhi mipira kwa Timu za JKU na Mafunzo.hafla hiyo imefanyika ukumbi wa VIP Amaan Zanzibar.
Mwenyekiti wa Kamati ya Muda ya ZFA Hussein Ali, akizungumza na Waandishi wa habari za Michezo Zanzibar wakati wa hafla ya kuwakabidhi Viongozi wa Timu za Mafunzo na JKU zinazoshiriki Michuano ya CAF, inayotarajiwa kufanyika mwezi ujao katika uwanja wa Amaan Zanzibar.
Mwenyekiti wa Kamati ya Muda ya ZFA Hussein Ali, akimkabidhi Kiongozi wa Timu ya Mafunzo Khamis Ali Machenga, mipira 10kwa ajili ya timu yake kujiandaa na Michuano ya Kombe la Klabu Bingwa Barani Afrika  inayotarajiwa kufanyika katika Uwanja wa Amaan Zanzibar Timu ya Mafunzo itaaza michuano hiyo na Timu ya AS Vita ya Congo, mchezo huo utafanyika katika uwanja wa Amaan tarehe 13/2/2016. katika uwanja wa Amaan Zanzibar. 
Mwenyekiti wa Kamati ya Muda ya ZFA Hussein Ali akimkabidhi mipira 10 kiongozi wa Timu ya JKU Saadu Ujudi, kwa ajili ya timu yake kujiandaa na Michuano ya Kombe la Washirikisho Barani Afrika mchezo utakaofanyika katika Uwanja wa Amaan Zanzibar tarehe 14/2/2016, ikicheza na Timu kutoka Botswana Timu ya Gaborone United. ili kuweza kujiandaa na michuano hiyo kwa kuwakilisha Zanzibar. 
Kiongozi wa Timu ya Mafunzo Khamis Ali Machenga akizungumza baada ya kukabidhiwa vifaa hivyo na kutowa shukrani kwa Kamati ya ZFA kwa msaada huo na kuahidi Timu yake kufanya vizuri katika mchezo wao huo wa kwanza wa Kombe la Klabu Bingwa Barani Afrika unaofanyika uwanja wa Amaan Zanzibar.
Kiongozi wa Timu ya JKU Afande Khamis Chibudi akitowa shukrani kwa Kamati ya ZFA kwa msaada wao huo na kuahidi itafanya vizuri katika mchezo wao huo wa Kombe Shirikishi itakayoaza na Timu ya Gaborone  ya Botswana utakaofanyika katika uwanja wa Amaan Zanzibar tarehe 14/2/2016.  
Waandishi wa Habari ya Michezo Zanzibar wakiwa katika hafla ya kukabidhiwa Vifaa vya Michezo Timu za JKU na Mafunzo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.