Habari za Punde

Kumekucha Dodoma Hapa Kazi Tu Half ya Marathon.

Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania ,Anthony Mtaka akiwa na Mwenyekiti wa Chama cha riadha mkoa wa Kilimanjaro,( KAA) Liston Methacha wakati wa uzinduzi rasmi wa mbio za Dodoma Hapa Kazi tu Half Marathoni 2016 zinzotarajia kufanyika January 30 mwaka huu mjini Dodoma.
Baadhi ya wadau wa Riadha wakifuatiia mkutano wa uzinduzi wa Mbio za Dodoma Hapa kazi tu Half Marathon 2016 uliofanyika katika Hotel ya Nyumbani mjini Moshi.
Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) Anthony Mtaka akizungumza na wanahabari (hawako pichani ) wakati wa uzinduzi rasmi wa Mbio hizo.
Kocha wa timu ya taifa ya Riadha ,Francis John akiwa na wanariadha ,Alphonce Felix na Said Makula waliofuzu viwango vya kushiriki mashindano ya Olyipiki ,walipotamburishwa mbele ya wanahabari .
Raisi wa RT ,Mtaka kifanya mahojiano na Mwandishi wa habari ,Enos Masanja wa Azam TV.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

Shirikisho la Riadha Tanzania(RT) limeandaa mbio fupi kwa ajili ya kuhitimisha siku 100 za rais Dk.John Pombe Magufuli kuwa Ikulu zitakazotimua vumbi jumamosi hii januari 30 mwaka  huu mjini Dodoma.

Mbio hizo zimepewa jina maalumu la Dodoma ‘hapa kazi tu’ Half Marathon ambazo zitashirikisha washiriki mbali  mbali wakiwamo waheshimiwa wabunge,mawaziri,wanafunzi,walemavu na wanariadha wakongwe nchini.

Akizindua mbio hizo mjini Moshi mwishoni mwa wiki zinazodhaminiwa na Kampuni ya JSM,Rais wa shirikisho hilo,Anthony Mtaka alisema kuwa lengo la kuanzishwa kwa mbio hizo ambazo zimeandaliwa na kuendeshwa na shirikisho hilo ni kufufua michezo hapa nchini.

Pia alisema mbio hizo zitatumika kwa ajili ya kumpongeza Rais Dk.John Pombe Magufuli kutimiza siku 100 tangu aingie maradakani ambazo zitakuwa februari 14 mwaka huu.

Kwa mujibu wa rais huyo wa RT,mbio hizo zimegawanywa katika makundi matatu ambako mbio za kwanza ni za kilomita 2.5 ambazo zitashirikisha wabunge,mawaziri,walemavu,wanafunzi ,wazee na watu mbalimbali.

Mbio za kilomita 5 ambazo ni za kujifurahisha zitashirikisha wakimbiaji wote na mbio za nusu marathon ambazo zitakuwa ni mbio za ushindani washindi watapata zawadi .

Akitangaza zawadi  kwa washindi,Mtaka alisema mshindi wa kwanza kwa upande wa wanaumme na 
wanawake atapata zawadi  ya piki piki yenye thamani ya sh,Milioni 2.8,mshindi wa pili akipata bati 100,wa tatu bati 40,mshindi wa nne akipata sh,200,000 huku mshindi wa tano akiondoka nash,100,000.

Mshindi wa sita hadi wa kumi watapata kifuta jasho cha sh,50,000 kila mmoja huku waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa  ndiye atayakuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa mbio hizo na atashiriki  mbio za kilomita 2.5.

Wanafunzi waatakaopenda kushiriki mbio hizo watasajiliwa kwa sh,500,huku vwasio wanafunzi wakisajiliwa kwa sh,1,000 na wingine ambao hawakutajwa ni kundi gani wakisajiliwa kwa sh,5,000 na fedha hizo kwa mujibu wa Mtaka zitasaidia kambi ya wanariadha watakaoshiriki michuano ya Olimpiki.

Uzinduzi huo pia ulitumika kuwatambulisha wanariadha wawili ambao wamekidhi vigezo vya kushiriki michuano ya Olimpiki itakayofanyika nchini Brazil mapema mwezi Agosti mwaka huu  ambako nchi zaidi ya 216  kutoka kila kona ya dunia zitashiriki.

Wanariadha hao ni Alphonce Felix ambaye ana wastani wa muda wa kukimbia wa saa 2:12.01 na Said Makula ambaye muda wake wa kukimbia ni saa 2:13.27 na watatumia mbio hizo mjini Dodoma kama majaribio yao ya kitaifa kati ya majaribio sita ya kitaifa kabla ya kwenda Brazil.

Julai 6 mwaka jana,Felix alishiriki mbio za Gold Coast Marathon nchini Australia na kumaliza nafasi ya sita huku Makula akishiriki mbio za Casablanca Marathon oktoba 25 mwaka jana  na kumaliza katika nafasi ya nne.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.