Naibu
Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Anastazia Wambura
(kulia) akiongea na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh.Said Meck Sadiki wakati wa
ziara ya Mh. Naibu Waziri aliyoifanya katika Wilaya ya Temeke kukagua viwanja
vya wazi vilivyokusudiwa kwa ajili ya michezo ambavyo vimemiwa na baadhi ya
wananchi
Naibu
Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Anastazia Wambura
(kulia) akiagana na Mkuu wa Mkoa wa Dar
es Salaam Mh.Said Meck Sadiki tayari kuanza ziara ya kukagua viwanja vya wazi
vilivyokusudiwa kwa ajili ya michezo vilivyovamiwa na baadhi ya wananchi
Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Mainispaa ya Temeke Bw.Waziri Kombo akimkabidhi
Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Anastazia
Wambura taarifa ya utekelezaji kuhusiana
na shughuli za Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo za Halmashauri hiyo, kulia
ni Mbunge wa jimbo la Temeke Mh.Abdalah Mtolea na kushoto ni Naibu Meya wa
Manispaa hiyo Mh.Salum Fesal.
Naibu
Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Anastazia Wambura wa
pili kutoka kulia akikagua Uwanja wa Tandika ambao una mgogoro na wapangaji wa
maduka ambapo aliagiza siku saba kwa wavamizi wote nchini kutoka kwenye viwanja
hivyo kwa ajili ya kupisha shughuli za michezo, wa pili kutoka kushoto ni Naibu
Meya wa Manispaa hiyo Mh.Salum Fesal
Mwenyekiti wa Bodi ya Mikono Arts
aliyesimama Bw.Henry Clemensi akiongea
na Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Anastazia
Wambura kuhusu shughuli wanazofanya ili kuwasaidia wasanii wa sanaa za
uchongaji ikiwa ni pamoja na kuwatafutia soko nje ya nchi, wa kwanza kulia
waliokaa ni Mbunge wa jimbo la Temeke Mh.Abdalah Mtolea na wa kwanza kushoto ni
Naibu Meya wa Manispaa hiyo Mh.Salum Fesal.
(Picha na Benjamin Sawe-WHUSM).
No comments:
Post a Comment