Habari za Punde

Wazazi Mkoani Mwanza Wasikitika na Elimu Bure Kuwabagua Wanafunzi wa Elimu ya Watu Wazima.

Wazazi na Walezi wa Wanafunzi wanaosoma kitengo cha elimu ya Watu Wazima katika Shule ya Sekondari Pasiansi iliyopo Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza, wameiomba Serikali kuondoa ada kwa wanafunzi hao ili nao waweze kunufaika na mpango wa elimu bure nchini.

Wazazi hao wametoa ombi hilo hii leo baada ya kumalizika 

kwa kikao baina yao na uongozi wa Shule hiyo pamoja na 

Kitengo cha Elimu ya Watu Wazima Mkoani Mwanza, 

sanjari na viongozi wengine akiwemo diwani wa Kata ya Pasiansi pamoja na Afisa elimu Sekondani katika Manispaa ya Ilemela.

Malalamiko yao yanafafanua kwamba, hawakuambiwa tangu 

awali kuwa watoto wao wanasoma elimu ya Watu Wazima, 

malalamiko ambayo hata hiyo yamekanushwa na Mkuu wa 

Shule hiyo Mwalimu Joseph Bangirana.

Awali wazazi hao walisema kuwa hawako tayari kulipa ada 

kwa ajili ya watoto wao wanaosoma katika shule hiyo, jambo 

lililomlazimu Malimi Joram ambae ni Mkufunzi Msaidizi 

kutoka Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima Mkoani Mwanza 

kueleza bayana kwamba, wanafunzi wa Elimu ya Watu 

Wazima hawanufaiki na mpango wa elimu bure nchini kwa 

kuwa Serikali haitoi ruzuku kwa ajili yao.

Ufafanuzi huo ukaungwa mkono na Mwalimu Juma 

Kasandiko ambae ni Afisa Elimu Sekondari katika Manispaa 

ya Ilemela.

Wakati ufafanuzi huo ukitolewa, mmoja wa wanafunzi 

wanaosoma katika shule hiyo ya Pasiansi akasisitiza suala la 

wao kuondolewa ada ili nao wanufaike na mpango wa elimu 

bure.

Kitengo cha Elimu ya Watu Wazima katika shule ya 

Sekondari Pasiansi, kilianzishwa Mwaka 2014 na kuanza 

kupokea wanafunzi waliomaliza darasa la Saba waliokuwa na 

ufaulu wa chini ya Wastani wa pinti 100 kwa lengo 

la kuwapa fursa ya kupata elimu ya Sekondari ambapo mbali 

na michango mingine, wanafunzi hao wanalipa ada ya 

Shilingi Laki Moja na Elimu Hamsini kwa mwaka.
Kikao Kikiendelea
Mwalimu Juma Kasandiko ambae ni Afisa Elimu Sekondari katika Manispaa ya Ilemela akitoa ufafanuzi kwa Wazazi juu ya suala la Elimu Bure nchini.
Malimi Joram ambae ni Mkufunzi Msaidizi kutoka Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima Mkoani Mwanza
Andrea Swai kutoka Elimu ya Watu Wazima Mkoani Mwanza akitoa ufafanuzi katika kikao hicho
Mwalimu Joseph Bangirana ambae ni Mkuu wa Shule Pasiansi Sekondari akitoa ufafanuzi katika kikao hicho
Diwani wa Kata ya Pasiansi Mhe.Japhesi Joel Rwehumbiza akitoa ufafanuzi wake. Amewapongeza wazazi kwa kufuatilia masuala ya elimu yanayowahusu
Mdau wa Elimu Mkoani Mwanza, Peter Matonyi akitoa mchango wake juu ya suala la elimu bure kwa wanafunzi wa elimu ya watu wazima
Mwenyekiti wa Mtaa wa Pasiansi Mkoani Mwanza, Emmanuel Masuka akifafanua jambo
Mmoja wa Wazazi akiwasilisha malalamiko yake juu ya suala la elimu bure kuwabagua wanafunzi wa elimu ya watu wazima
Mmoja wa Wazazi akiwasilisha malalamiko yake juu ya suala la elimu bure kuwabagua wanafunzi wa elimu ya watu wazima
Wanalalamikia suala la elimu bure kuwabagua wanafunzi wa elimu ya watu wazima
Elimu bure inawabagua wanafunzi wa elimu ya watu wazima
Elimu bure inawabagua wanafunzi wa elimu ya watu wazima
Kutoka Pasiansi Sekondari Jijini Mwanza, Mimi ni Mzee wa Karanga fotoooooooo, GB Pazzo wa Binagi Media Group

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.