Habari za Punde

Ligi Kuu ya Zanzibar Mtende na Chuoni Mchezo Uliofanyika Uwanja wa Amaan Timu ya Mtende imeshinda 2--1

Beki wa Timu ya Mtende Rangers akiokoa mpira huo wakati washambuliaji wa timu ya Chuoni wakiwa tayari wakati wa mchezo wao wa Ligi Kuu ya Zanzibar uliofanyika uwanja wa Amaan Zanzibar Timu ya Mtende Rangers imeshinda mchezo huo kwa mabao 2--1.na kufikisha pointi 6 kwa kucheza michezo 13 ya ligi ya Zanzibar. hadi sasa. 
Beki wa Timu ya Mtende akiondoa mpira galini kwake.
Beki wa Timu ya Mtende na Mshambuliaji wa timu ya Chuoni wakiwania mpira wakati wa mchezo wao wa Ligi Kuu ya Zanzibar uliofanyika katika uwanja wa Amaan Zanzibar.
Bao la kwanza la timu ya Chuoni wakati wa mchezo huo wa ligi kuu ya Zanzibar. 
Mfungaji wa bao la kwanza la timu ya Chuoni akichangilia bao lake wakati wa mchezo huo na timu ya Mtende Rangers na kukubali kipigo cha mabao 2-11 dhidi ya timu ya Mtende Rengers uliofanyika uwanja wa Amaan Zanzibar.
Mshambuliaji wa timu ya Chuoni akiruka kihuzi cha beki wa timu ya Mtende wakati wa mchezo wao.
Mshambuliaji wa timu ya Mtende akipiga mpira golini kwa timu ya Chuoni wakati wa mchezo wao wa ligi kuu ya Zanzibar uliofanyika uwanja wa Amaan Zanzibar Timu ya Mtende imeshinda mchezo huo ukiwa mchezo wake wa mwazo kushinda katika ligi hiyo ya Zanzibar ikiwa na point 6, baada ya kucheza michezo 13.

Mchezaji wa timu ya Chuoni akimiliki mpira wakati wa mchezo huo huku beki wa timu ya Mtende akiwa tayari kumzuiya.
Goli la kwanza la timu ya Mtende katika mchezo huo na timu ya Chuoni uliofanyika uwanja wa Amaan Zanzibar.
Mchezaji wa timu ya Mtende akimpita beki wa timu ya Chuoni wakati wa mchezo huo. 
Muamizi wa mchezo huo Eddy akimuonesha kadi nyekundi nahodha wa timu ya Chuoni baada ya mchezo mbaya aliomchezea mchezaji wa timu ya Mtende wakati wa mchezo huo.





Mchezaji wa timu ya Mtende na Chuoni wakiwania mpira wakati wa mchezo wao wa ligi kuu ya Zanzibar uliofanyika uwanja wa Amaan Zanzibar.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.