Habari za Punde

Viongozi wa Asasi za Kiraia Kisiwani Pemba Wapata Mafunzo ya Elimu ya Uraia.

Afisa Mdhamini Wizara ya Katiba na Sheria Pemba,Ndg. Omar Khamis Juma, akifungua mafunzo ya elimu ya uraia kwa viongozi na wanachama wa asasi za Kiraia za Mkoa wa kaskazini Pemba, yalioandaliwa na Kituo cha Hudumza za Sheria Zanzibar tawi la Pemba, kulia ni Mratibu wa Kituo hicho Fatma Khamis Hemed pia mafunzo hayo yalifanyika afisini kwao mjini Chakechake
Mtoa Mada Bi.Fatma Khamis Hemed, akimuuliza mmoja wa viongozi wa asasi ya kiraia kutoka Mkoa wa Kaskazini Pemba, kwenye mafunzo ya elimu ya uraia, yaliondaliwa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, na kufanyika afisini kwao mjini Chakechake
Baadhi ya Viongozi wa Asasi za Kiraia Mkoa wa Kaskazini Pemba, wakisikiliza uwasilishaji wa mada kadhaa, kwenye mafunzo ya elimu ya uraia, yalioandaliwa na kufanyika Kituo Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba
Mtoa Mada Ndg. Khalfan Amour Mohamed kutoka Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, akiwasilisha mada kwenye mafunzo ya elimu ya uraia kwa NGOs za Mkoa wa Kaskazini Pemba,  yaliondaliwa na kufanyika ZLSC afisini kwao mjini Chakechake
Afisa Uhamiaji Mkoa wa Kasakzini Pemba Ndg.Omar Said Mohamed, akiwasilisha Mada ya Uraia, kwenye mafunzo ya elimu ya uraia, yalioandaliwa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC Tawi la Pemba, kulia ni mratibu wa mafunzo hayo Mohamed Hassan Ali, (Picha na Haji Nassor, Pemba).

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.