Habari za Punde

Jopo la Ngazi ya Juu Kuhusu Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi Lazinduliwa.

 Wenyekiti -Wenza wa Jopo la Ngazi ya Juu kuhusu  Uwezeshaji wa wanawake kiuchumi, Rais wa Costa Rica,  Mhe. Luis Guillerma Solis na Mkurugenzi Mtendaji wa  IKEA Switzerland Bi. Simona Scarpaleggia wakibadilishana mawazo na  Mwenyekiti wa Kundi la Nchi za Afrika katika Umoja wa Mataifa  Balozi Tuvako Manongi, mara baada ya kundi hilo kuzinduliwa rasmi na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, mapema wiki hii. Mmoja wa wajumbe wa Jopo ambao idadi yao ni 21 ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe. Samia Hassan Suluhu. Ban  Ki Moon ameunda Jopo  hilo  ili  limpatie maoni na mapendekezo kuhusu uwezeshwaji wa mwanamke kupitia utekelezaji wa Agenda 2030 ya Maendeleo Endelevu
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akiwa na  wenyeviti- wenza wa Jopo a  ngazi ya juu kuhusu  uwezeshaji wa wanawake kiuchumi pamoja na   baadhi ya wajumbe wa Jopo siku ya uzinduzi wa Jopo  hilo uliofanyika sambamba na  mkutano wa 60 wa  Kamisheni  ya Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya Wanawake (CSW) unaoendelea hapa Umoja wa Mataifa

Na MwandishiMaalum, New York

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, amezindua Jopo la Nganzi ya Juu ambalo ameliunda kusaidia kufanya uchambuzi na kutoa mapendekezo ya namna ya kuchagia kasi ya kuwawezesha Wanawake Kiuchumi.

Jopo hilo ambalo linaundwa na viongozi na wataalamu wa kada mbalimb

ali linaongozwa naWenyeViti-Wenza ambae ni Rai swa  Costa Rika,Mhe. Luis Guillerma Solis na Bi. Simona Scarpaleggia ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa  IKEA Switzerland.

Wajumbe wa Jopo ni pamoja na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Hassan Suluhu, Mkuu wa Banki ya Dunia,  Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Fedha (IMF) Mkurugenzi Mkuu wa ILO,  Mkurugenzi Mtendaji wa UN- 

WOMEN, wapo pia  Maprofessa na wataalamu wa uchumi, watafiti, viongozi wa vyama vya wafanyakazi, wawakilishi kutoka serikalini,wataalamu wa masuala ya jinsia na fursa sawa na wafanyabiashara. Kwa pamoja na jopo hilo linakuwa na wajumbe  21.

Mara baada ya kuzinduliwa rasmi kwa Jopo hilo, Marchi 15 

sambamba na Mkutano wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa 

kuhusu hali ya wanawake. 

Wenyeviti-Wenza walianza ratiba ya kukutana na Wenyeviti wa Makundi ya Kikanda ya Nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kwa madhamuni ya kupata ushauri na mawazo yao yalihusu mapendekezo ya Jopo hilo linatakiwa kuzingatia katika utafiti wake na hatimaye kile kitakacho ingizwa kwenye andiko lao.

Mwenyekiti wa Kundi la nchi za Afrika,  kwa mwezi Marchi, 

Balozi Tuvako Manongi alikuwa miongini mwa wenyeviti 

waliokutana na wenye-viti wenza wa Jopo,ambapo aliwasilisha baadhi ya maeneo ambayo Afrika inaamini kwamba yakiendelea kutiliwa mkazo yatachagia zaidi kasi ya kuwainua wanawake kiuchumi.

Baadhi ya maeneo hayo ni fursa ya wanawake kupata elimu pamoja na elimu ya juu, upatikanaji wa mitaji na mikopo,nafasi za uongozi zikiwamo za kisiasa,umiliki wa mali na haki ya kumiliki ardhi,afya ya uzazi na uzazi wa mpango na salama,kuondokana na umaskini na affirmative action na fursa za kupata misaada na ushauri wa kisheria.

Balozi Manongi amewaeleza wenye-vita 

wenza wa Jopo kuwa mapendekezo anayowasilisha kwa niaba ya 

nchi za Afrika si jipya kwani yanaendelea kufanyiwa kazi na serikali mbalimbali. Lakini ni Imani ya Afrika kwamba kama yakiendelea kupewa msukumo unaostahili pamoja na mengine yatakayokuwa yanawasilishwa kwa Jopo bila shaka kasi ya uwezeshwaji wa wanawake kiuchumi itakuwa kubwa zaidi.

Jukumu  la  Jopo hilo la 

Uwezeshwaji wa Wanawake kiuchumi pamoja na  mambo 

mengine ni kutoa mapendekezo kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa 

Mataifa juu ya uwezeshwaji wa wanawake kupitia utekelezaji wa Ajenda 2030 ya Maendeleo Endelevu kwa kuboresha matokeo ya kiuchumi kwa wanawake, kupaisha uongozi wa wanawake katika kusukuma mbele ajenda 2030 ambayo ni jumuishi, endelevu na inayojali mazingira.

Vile vile Jopo litatakiwa kutoa mapendekezo ambayo watendaji na watoa maa muzi serikalini, katika sekta binafasi, Taasisi za Umoja wa Mataifa, na wadau wengine wataweza kuyafanyia kazi. Ripoti ya kwanza Jopo inatarajiwa kuwasilishwa mwezi Septemba
2016.





No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.