Na: Abdi Suleiman, PEMBA.
Katika hali isiyo ya kawaida wachezaji wanne wa
timu ya Yanga, wameshindwa kufanya mazoezi na
wenzao kwa sababu mbali mbali.
Yanga ambayo ipo Pemba kwa ajili ya maandalizi ya
mchezo wao na Azam FC wa ligi kuu ya
sokaTanzania bara, utapigwa katika uwanja wa taifa
wikiendi hii.
Wachezaji hao ambao wameshindwa kuungana na
wenzao ni Saimon Msuva, Salum Telela, Nadir
Haroub Kanavaro na Amis Tambwe ambaye
hakuonekana kabisa kiwanjani hapo.
Saimon Msuva na Salum Telela waliweza kuungana
na wenzao katika kuomba dua, badala yake wakakaa
pembeni na kuwaachia wenzao kuendelea na
program zao, huku kocha mkuu Hans Van Plujin
akiwataka kukimbia uwanjani humo.
Saimon Msuva alilazimika kukaa chini baada ya
kushindwa kuendelea na mazoezi mepesi ya
kukimbia na kumwacha Telela akimaliza raundi
zisizopungua 15.
Kufuatia hali ya majeruhi kuanza kuindama Yanga,
imemfanya kocha wa timu hiyo kuwa makini katika
mazoezi yanayoendelea katika uwanja wa Gombani.
Wakati huo huo timu hiyo imelazimika kubadilisha
ratiba ya mazoezi iliyokuwa ikiifuata kila siku tokea
kuwasili kisiwani Pemba, ambapo leo timu hiyo
imefanya mazoezi yake asubuhi majira ya saa nne
kamili kijuwa kikali kikiwaka.
Yanga imeonekana kuukamia vikali sana mchezo huo
dhidi ya Azam, kwani inataka kujihakikishia
inawakimbia kwa masafa marefu wapinzani wao,
huku kesho baada ya mazoezi inatarajiwa kuondoka
kisiwani Pemba kurejea Tanzania bara.
No comments:
Post a Comment