Habari za Punde

Meli Kubwa ya Kitalii MS Hamburg Yafunga Gati Bandari ya Zanzibar leo 21/3/2016.

Meli ya Kitalii ya MS Hamburg yafunga gati katika bandari ya Zanzibar, 21/3/2016, ikiwa na Watalii 400 kutoka mataifa mbalimbali Duniani ikiwa katika bandari ya Zanzibar na Watalii hao kutembelea sehemu mbalimbali za kihistoria za Unguja ikiwa Zanzibar kwa siku moja, meli ya kisasa ya kitalii inayomilikiwa  na Conti Group na husimamiwa safari zake na Plantours Kreuzfahrten pamoja na na Ocean Tours ikiwa ni sehemu kampuni ya Akorn group (a division of Abercrombie & Kent). Meli hii mara ya mwisho kuja Zanzibar na Wataii ilikuwa mwaka 2014. 
Watalii wakiwa katika Bandari ya Zanzibar wakatika kuelekea kutembelea sehemu za Historia ya Visiwa vya Unguja. Zanzibar ni moja ya Nchi za Afrika Mashariki zikiwa na Historia.  

Watalii wakiwa katika Bandari ya Zanzibar wakipata bidhaa kutoka kwa Wajasiriamali wa Bidhaa za Kitalii Zanzibar. 
Meli kubwa ya kitalii MS Hamburg imetia nanga bandari ya Zanzibar leo asubuhi ikiwa na watalii zaidi ya 400. Ilitarajiwa kuondoka jioni ya leo na kuendelea na safari yake.

Watalii hawa walishuka melini na kufanya safari za matembezi katika sehemu tofauti za kihistoria za mji wa Zanzibar na vitongoji vyake.

MS Hamburg ni meli ya kisasa ya kitalii inayomilikiwa  na Conti Group na husimamiwa safari zake na Plantours Kreuzfahrten pamoja na na Ocean Tours ikiwa ni sehemu kampuni ya Akorn group (a division of Abercrombie & Kent).



No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.