Habari za Punde

Sherehe za Kuapishwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DkAli Mohamed Shein Uwanja wa Amaan Zanzibar leo 24-3-2016.Bwaride Maalum lililoandaliwa na Vikosi vya Ulinzi na Usalama kwa ajili ya hafla ya kumuapisha Rais Mteule wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein. vikiwa katika uwanja wa Amaan kwa ajili ya shughuli hiyo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Rais Mteuli Dk Ali Mohamed Shein , akiingia Uwanja wa Amaan kwa msafara Maalum wa Pikipiki za Polisi zikimshindikiza katika hafla hiyo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Rais Mteuli Dk Ali Mohamed Shein , akiingia Uwanja wa Amaan kwa msafara Maalum wa Pikipiki za Polisi zikimshindikiza katika hafla hiyo ya kuapisha iliofanyuika katika uwanja huoa 
Rais Mteule wa Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza  la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiwasili katika Uwanja wa Amaan Zanzibar kwa ajili ya Kuapishwa. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akielekea katika jukwaa kupokea salama na kupigiwa mizinga 21 ya kuashiria kumasliza kwa kikomo cha uongozi wake wa kipindi cha miaka mitano.  
Vikosi vya Ulinzi na Usalama vikioa heshima wakati wa kupigwa mizinga 21 ya kumuaga Rais wa Zanzibar baada ya kumaliza kipindi chake cha kwanza cha miaka mitano ya Uongozi wa Urais wa Zanzibar na kuapishwa tena baada ya kushinda Uchaguzi wa Marudio uliofanyika wiki iliokwisha.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi akikagua bwaride maalum lililoandaliwa kwa ajili yake katika uwanja wa amaan wakati wa hafla ya sherehe za kuapishwa.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti Baraza la Mapinduzi Dk  Ali Mohamed Shein, akikaguwa bwaride Maalum lililoandaliwa kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza kipindi chake cha miaka mitano. na kuapishwa tena kwa kipindi cha pili cha uongozi wake baada ya kushinda Uchaguzi wa Zanzibar uliofanyika jumapili 20/3/2016.Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akikaguwa bwaride maalum lililoandaliwa kwa ajili yake.


Maandamano ya Majaji wakiongozwa na Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe Omar Othman Makungu wakielekea katika jukwaa la kuapishwa Rais Mteuli wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, zilizofanyika katika Uwanja wa Amaan Zanzibar, akiongozana na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Pandu Ameir Kificho.
Wawakilishi wateule wakiwa katika jukwaa wakihudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, katika viwanja vya Amaan Zanzibar.
Rais Mteule wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, akila kiapo cha Utii wa Urais wa Zanzibar wakati wa hafla hiyo ya kumuapisha iliosimamiwa na Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu, katikati Katibu Mkuu Kiongozi Dk Abdulhamid Yahya Mzee.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akitia saini hati ya kiapo baada ya kukamilika kwa taratibu hiyo. 
Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe Omar Othman Makungu akiweka saini hati ya Kiapo ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi baada ya kumalizika kwa hafla hiyo iliofanyika uwanja wa Amaan Zanzibar.
Kadhi Mkuu wa Zanzibar Shekh. Khamis Haji Khamis, akisoma dua baada ya hafla ya kumuapisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, iliofanyika katika Uwanja wa Amaan Zanzibar.
Askofu wa Kanisa Katoliki Zanzibar, Askofu Augustino Shao akisoma dua baada ya hafla ya kumuapisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, iliofanyika katika Uwanja wa Amaan Zanzibar.
Askofu wa Anglikana Jimbo la Zanzibar  Askofu Hafidh, akisoma dua baada ya hafla ya kumuapisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, iliofanyika katika Uwanja wa Amaan Zanzibar.
Viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakifuatilia sherehe za kumuapisha Rais wa Zanzibar katika Uwanja wa Amaan Zanzibar.
Mabalozi Wanaoziwakilisha Nchi zao Tanzania wakifuatilia hafla hiyo ya Kuapishwa kwa Rais wa Zanzibar katika Uwanja wa Amaan Zanzibar.

Jopo la Majaji likiongozwa na Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu wakirudi katika sehemu zao baada ya kumalizika kwa hafla ya Kiapo cha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,

Viongozi wa Madhehebu ya Dini Zanzibar, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Mhe Jecha S Jecha na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama Zanzibar wakirudi katika sehemu zao jukwaa kuu baada ya kumalizika kwa hafla ya kumuapisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein. 
Viongozi wa Jukwaa kuu wakiwa wamesema wakati wa kutowa heshima kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kupigwa wimbo wa Taifa na kupigwa mizinga 21 ya kuingia madarakani baada ya kuapishwa, kwa kipindi cha Pili cha Uongozi wake wa Urais wa Zanzibar. 

Gwaride Rasmin la Vikosi vya Ulinzi na Usalama Zanzibar likiwa katika umbile la Alpha kwa ajili ya kukaguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, lililofanyika katika Uwanja wa Amaan Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akikagua bwaride rasmin baada ya kumaliza kula kiapo cha Urais wa Zanzibar. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.