Habari za Punde

Washauriwa kuanzisha English Club

Na Salmin Juma, Pemba

Mkuu wa mkoa wa Kaskazini Pemba , Mhe Omar Khamis Othman amewashauri walimu wakuu katika Wilaya ya Micheweni  kuanzisha English  Club ili kuwaandaa wanafunzi kwa ajili ya kufanya kazi katika hoteli za kitalii .

Amesema ni vyema walimu hao hususani wanaotoka maeneo ya uwezekaji kuzitumia fursa zilizopo  kwa kujenga uwezo wa  wanafunzi  wa kujua kuzungumza kiingreza ili kuwafanya wanufaike na uwepo wa sekta ya utalii katika maeneo yao .

Akizungumza na walimu Wakuu wa Skuli za Msingi na Sekondari Wilaya  hiyo kwenye ukumbi wa chuo cha walimu Wingwi , Mkuu huyo ameeleza kufurahishwa na hatua iliyofikiwa na Jumuiya ya Maendeleo ya Elimu Zanzibar (ZEDO) kuanzisha English Club pamoja na English class kwa baadhi ya Skuli za Zanzibar .

Amefahamisha kuwa uwamuzi wa kuanzishwa English Club pia kutasaidia kuongeza ufaulu wa wanafunz katika mitihani yao ya Taifa kwani watakuwa na uwezo ya kujibu vyema mitihani kwa umakini .

Mapema akizungumza kwenye mkutano huo , Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo ya Elimu Zanzibar (ZEDO) Ussi Said Suleiman amesema kwamba Jumuiya hiyo imekuwa ikitoa mbinu bora za upasishaji wa wanafunzi kupitia sekta ya michezo na sanaa.

Amesema kupitia mbinu hiyo wameweza kuwarudisha skuli wanafunzi waliokuwa wameacha masomo kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo ukosefu wa vifaa na sare .

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.