Habari za Punde

ZAPSWU yaagiza kushirikiana na kufanya kazi kwa uadilifu

Na Salmin Juma Pemba

Chama cha Wafanyakazi wa Huduma za Umma Zanzibar  {ZAPSWU} kimewasisitiza Makatibu wa matawi wa Chama hicho kushirikiana kwa pamoja na kufanya kazi kwa uadilifu na kuyasikiliza malalamiko ya yanayotolewa na wanachama wa chama chao ili kuweza kuyafikisha malalamiko hayo  kwa  viongozi  wa juu.

Ushauri huo umetolewa na naibu katibu mkuu wa chama hicho Suleiman Juma Suleiman wakati alipokuwa akizungumza na makatibu wa matawi wa chama hicho huko katika ukumbi wa Maktaba Chake Chake Pemba.

Amesema kuwa  amebaini  kutokuwepo na ushirikiano wa kutosha kati ya makatibu na wanachama wengine ambapo kumepelekea  kushindwa kutekeleza wajbu na majukumu yao kwa pamoja .

Aidha amewataka makatibu hao kuhakikisha kwamba wanakiimarisha chama hicho ili kuongeza nguvu  mpya za upatikanaji wa wanachama wapya katika chama hicho

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.