Habari za Punde

Wizara ya Habari mabingwa kombe la michuano ya kuadhimisha siku ya kisukari duniani

 Wachezaji wa Timu ya soka ya Wizara ya Habari jezi (bluu) wakisalimiana na wachezaji wa timu ya Wizara ya Elimu kabla ya pambano la fainali la kombe la maadhimisho ya kisukari duniani lililofanyika uwanja wa Amani. Katika pambano hilo Habari ilishinda mabao 4-3.
 Mshambuliaji Yussuf Saleh wa timu ya Habari akimtoka mlinzi wa timu ya Elimu Shaaban Naimu katika pambano la fainali la kombe la kisukari lililofanyika uwanja wa Amani, Habari ilishinda mabao 4-3.

 Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo (katikati) akifuatilia pambano la fainali la kombe la kisukari kati ya timu ya Wizara ya Habari na Wizara ya Elimu lililofanyika Uwanja wa Amani Mjini Zanzibar.

 Waziri Mahmoud Thabit Kombo akimkabidhi kombe la mashindano ya kisukari nahodha wa timu ya Wizara ya Habari Mussa Abdlaa (fujo) baada ya kuilaza Elimu mabao 4-3 katika mchezo wa fainali ulifanyika Uwanja wa Amani Mjini Zanzibar.
Mabingwa wa kombe la kisukari timu ya Wizara ya Habari wakiwa katika picha ya pamoja na kombe la walilonyakuwa la michuano ya kisukari yaliyoshirikisha Wizara nane za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Picha na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.