Habari za Punde

Kikosi cha URA Wasogea Visiwani Zanzibar Kushiriki Kombo la Mapinduzi Cup Wakiwa Mabingwa Watetezi wa Kombe Hilo.

Mabingwa watetezi wa Kombe la Mapinduzi klabu ya URA watamkosa mlinzi wao tegemeo Richard Kasagga na kiungo Feni Ali katika mbio za kutetea ubingwa wao.


Kocha mkuu wa kikosi hicho Kefa Kisala alisema wanandinga hao watakosekana kutokana na kuwa majeruhi kwa mlinzi huyo huku kiungo Feni Ali akiwa na matatizo ya kifamilia.
Hata hivyo kocha huyo alisema anaamini wachezaji waliobakia kwenye kikosi hicho wataweza kuutetea ubingwa wao huku pia akiamini watapata mazoezi ya kutosha kwa ajili ya kurejea kwenye ligi kuu nchini Uganda mwezi February.

Wawakilishi hao wa Uganda wamepangwa kundi A wakiwa na Simba kutoka Tanzania bara, KVZ, Taifa Ya Jang’ombe na Jang’ombe Boys zote kutoka Zanzibar.

Kikosi cha URA kilichosafiri asubuhi ya leo kuelekea Zanzibar kinaundwa na:

Walinda mlango: Alionzi Nafian Legason na Allan Owiny
Walinzi: Fred Okot, Julius Ntambi, Samuel Sekitto, Jimmy Kulaba (C) na Allan Munaaba

Viungo: Richard Wandyaka, Shafik Kagimu, Jimmy Lule Kibirige, Nicholas Kagaba, Julius Mutyaba, Hood Mulikyi na Elkanah Nkugwa
WashambuliajiRobert Mukongotya, Bokota Labama Kamana, Ronald Kigongo na Villa Oromchan

Viongozi:
Kefa Kisala (Head Coach), Sadiq Wassa (Assistant coach), Simeon Massa (Trainer), Joseph Lubega (Team Doctor), Godfrey Ndugga (Ass. Manager), 

Geoffrey Masozi (Team Manager), Edward Kulubya (C.E.O), Fred Mwanjuzi (Team Security Officer) na Geoffrey Kyondo (Leader of Delegation).

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.