Habari za Punde

Mama aliyemuua mwanawe kisiwani Pemba nae afariki dunia

Na Mwandishi wetu Pemba

Mwanamke aliekamatwa na polisi kwa tuhuma za kumuua mtoto wake katika kijiji cha Wingwi Micheweni Pemba  nae amefariki dunia  huku Polisi na Hospitali wakitupiana mpira kuhusu mazingira ya kifo chake.

Jeshi la Polisi ambao walikuwa wakimshikilia mwanamke huyo wamesema alifariki akiwa Hospiltalini  lakini madaktari wamesema walipompokea  mwanamke huyo kutoka kwa Polisi akiwa tayari amefariki dunia.

Kamanda wa polisi mkoa wa kaskazini Pemba, Haji Khamis Haji  amesema waliamua kumpelaka hospitali mwanamke huyo baada kusema amebanwa na mafua ili ende kupatiwa matibabu.

Daktari aliyemfanyia uchunguzi marehemu huyo, Dk Khalfan Said Salum  amesema wamempokea mwanamke huyo kutoka kwa jeshi la polisi  akiwa tayari  ameshafariki dunia.

Amesema wakati anaendelea kumpima  marehemu hyo walimkuta akiwa ametokwa na povu jingi mdomoni na hiyo kuchukua sampuli kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Hata hiyo mwandishi wa habari hizi akiwa anatoka katika hospitali ya Micheweni  amemuona mtuhumiwa wa pili wa tukio hilo akiwa   anapelekwa hospitali kwa kupatiwa matibabu akiwa na ulinzi kutoka jeshi la Polisi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.