Habari za Punde

Mwengine Serengeti Boys , Hussein Deco apiga hodi mjini Unguja

 Hussein Deco alipokuwa akitekeleza majukumu yake akiwa na Timu ya taifa ya Vijana Serengeti Boys
SASA WAMEPANIA KUTETEA TAJI LAO LA ROLLING STONE

Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.

Mabingwa  watetezi wa Mashindano ya Vijana ya Rolling Stone kombain ya Mjini Unguja wamepania kutetea taji lao baada ya kuzidi kuimarisha kikosi chao kufuatia ujio wa kiungo mshambuliaji wa timu ya Kilimani City Assad Juma “Hussein Deco” ambae asubuhi ya leo kwenye uwanja wa Amaan ameanza mazoezi.

Hussein Deco  amerejea Visiwani Zanzibar hivi karibuni akitokea mjini Gentil, nchini Gabon katika michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya AFCON akiitumikia timu ya Taifa ya Tanzania “Serengeti Boys” baada ya kutolewa kwa kufungwa 1-0 na Niger katika mchezo wa mwisho wa Kundi B Uwanja wa Port Gentil mjini Gentil, nchini Gabon.

Huyo ni mchezaji wa pili kwenye timu hiyo ya Mjini Unguja mwenye uzoefu wa kucheza mashindano makubwa ya AFCON kufuatia juzi Mshambuliaji wa Klabu ya Miembeni City, Ibrahim Abdallah “Imu Mkoko” kujumuika na wenzake hao ambao  wanatarajia kwenda jijini Arusha mwezi July mwaka huu kwenye Mashindano ya Vijana ya Rolling Stone.

Kikosi cha Mjini Unguja (Mabingwa watetezi) mpaka sasa kina jumla ya wachezaji 26 wakiwemo walinda mlango Aley Ali Suleiman “Manula” (Miembeni city), Peter Dotto Mashauri (Schalke 04) na Makame Mkadar Koyo (Huru).

Wachezaji wa ndani ni Muharami Khamis “Terra” (Black Sailors), Abdul hamid Salum “Ramos” (KVZ), Ali Juma Maarifa “Mabata” (Taifa ya Jan’ombe), Hassan Chalii (Kipanga), Abdul-halim Ameir (King Boys), Shaaban Pandu (Villa United), Idrissa Makame (Villa FC), Ramadhan Simba (Calypso), Ali Hassan (Uhamiaji), Fahmi Salum (Mlandege), Salum Omar (Villa United), Yakoub Omar (Jang’ombe Boys) na Mohd Ridhaa (Villa United).

Wengine ni Mohd Jailan (Chrisc), Makame Masoud (Schalke 04), Mohd Mussa (Mapembeani), Abrahman Juma (KMKM), Mohd Haji (Jang’ombe Boys), Abdul-hamid Juma (ZAFSA), Ibrahim Chafu (Villa FC) na Juma Ali Yussuf “James” (Villa United).

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.