POLISI wa usalama barabarani
wakiwa kwenye zoezi maalum la kufanya uhakiki wa bima halali kwa njia ya
mtandao, mara baada ya Polisi hao kupata mafunzo ya jinsi ya utambuzi wa bima
zia kughushi, hivi karibuni kisiwani Pemba, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
MTOTO Fauzi Mohamed Subeit (16) mkaazi wa Mkoroshoni
wilaya ya Chakechake, akizungumza na waandishi pamoja na Polisi wa usalama
barabarani, baada ya kukamatwa akiendesha gari kinyume na sheria, wakati Polisi
hao wakifanya uhakiki wa bima halali kw anjia ya mtandao, mara baada ya Polisi
hao kupewa mafunzo na Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania TIRA, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
MKUU wa kikosi cha uslama
barabarani mkoa wa kusini Pemba Shawali Abdalla Ali, akishiriki katika zoezi la
utambuzi wa bima halali, akiwa na watendaji wengine kutoka Mamlaka ya Usimamizi
wa Bima Tanzania ‘TIRA’ ambapo vyombo vya usafiri 71 walivigundua havina bima
halali katika 168 walivyovihakiki, (Picha
na Haji Nassor, Pemba)
BAADHI ya abiria walikuwa
wakisafiri na gari mbali mbali za abiria, wakilazimika kutembea kwa miguu
wakiwa na mizigo yao, baada ya gari walizokuwa wamepanda kufanyiwa uhakiki wa
bima zao na kugundulika kuwa ni za kughushi, kwenye zoezi maalumu lililofanywa
na Jeshi la Polisi na Mamlaka ya usimamizi wa bima Tanzania TIRA, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
WATENDAJI wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania TIRA, wakilifanyia uhakiki gari linalomilikiwa na Kampuni na Bakhersa Food Products, iwapo bima yake inatambulika, wakati wa zoezi hilo maalum lililofanyika hivi karibuni kisiwani Pemba, (Picha na Haji Nassor, Pemba)
No comments:
Post a Comment