Habari za Punde

Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wazee Vijana Wanawake na Watoto Zanzibar Mhe. Maudline Castico Azindua Mpango Kazi wa Kutokomesha Udhalilishaji Zanzibar.


Waziri wa Kazi Uwezeshaji wa Wazee Vijana Wanawake na Watoto Zanzibar Mhe. Maudline Castico akihutubia na kuzindua Mpango Kazi wa Ukatili Udhalilishaji dhidi ya Wanawake na Watoto Zanzibar, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar.
Wadau wakifuatilia hafla hiyo ya Uzinduzi wakimsikiliza Waziri Maudline Castico akizindua Mpango huo.
Mwakilishi wa Shirika la Kusaidia Watoto la UNICEF Bibi. Maniza Zaman akimuwakilisha Mkaazi wa Umoja wa Mataifa Nchini Tanzania, akisoma Ujumbe wa Masharika ya Umoja wa Mataifa wakati wa uzinduzi huo wa mpango kazi wa kutokomeza udhalilishaji wa Wanawake na Watoto Zanzibar uzinduzi huo umefanyika katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar.
Mtoto Jaffar Ahmada akisoma Ujumbe wa Watoto wa Zanzibar wakati wa Uzinduzi huo uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar.  
Mwakilishi wa Wanawake Zanzibar Bi. Fatma Abdalla Mussa akisoma Ujumbe wa Watoto wa Zanzibar wakati wa Uzinduzi huo uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar. No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.