Habari za Punde

Muamuzi na Mchezaji wa Zamani wa Timu ya Jeshi na Kikwajuni Zanzibar Marehemu Ahmed Awadh Marungu Afariki Dunia. Ni Pigo Kwa ZFA na Wapenzi wa Soka Zenj

Innaa LIllaahi wainaa ilayhi Raajiuun

Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.

Muamuzi mstaafu wa Kimataifa Ahmed Mohd Awadh (Mzee Marungu) amefariki dunia leo Jumanne Agost 22, 2017 ambapo Maziko yatafanyika nyumbani kwake Shangani na kuzikwa leo saa 7 mchana Mwanakwerekwe.

Mbali ya kuwahi kuwa muamuzi wa kimataifa pia marehemu alikuwa Kamisaa wa ligi za Zanzibar.

Juzi wapenzi wa soka Visiwani Zanzibar walipata pigo jengine kufutia kuondokewa na Dokta wa zamani wa timu ya Taifa ya Zanzibar “Zanzibar Heroes” Dokta Abdallah Said Mohammed “ Dokta Kuku” aliyefariki dunia Agosti 20, 2017 nyumbani kwake Muembetanga mjini Zanzibar na kuzikwa jana Agost 21, 2017 kijijini kwao Fujoni Wilaya ya Kaskazini ‘B’ Unguja.

Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu mahala pema Peponi Amiin.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.