Habari za Punde

Gulioni yaanza kwa kishindo Wilaya ya Mjiini yaitandika Dira 5-0


Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.

Timu ya Soka ya Gulioni FC imeanza vyema ligi daraja la Pili Wilaya ya Mjini baada ya kuitandika Dira FC mabao 5-0 kwenye mchezo uliopigwa saa 8 za mchana katika uwanja wa Amaan.

Mabao ya Gulioni yamefungwa na Maulid Salum Abdallah akipiga Hat trick dakika ya 14, 48 na 88 huku mabao mengine yakifungwa na Haji Juma Ali dakika ya 22 na 24.


Ligi hiyo itaendelea tena kesho kwa kupigwa michezo miwili katika uwanja wa Amaan.

Saa 8:00 za mchana wataanza Shangani dhidi ya Gereji, na saa 10:00 za jioni watasukumana kati ya Kundemba dhidi ya Muembe Makumbi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.