Habari za Punde

Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Azungumza na Maofisa wa Zanzibar Leo Pemba.

Mdhamini wa Shirika la Magazeti ya Serikali Pemba , Bakar Mussa Juma,akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba,juu ya dhamira ya Shirika hilo kufanya ziara ya kuangalia shughuli mbali mbali zinazofanywa na taasisi za Serikali mkoani humo .
Katibu Tawala Mkoa wa Kaskazini Pemba, Ahmed Khalid Abdalla,akizungumza mbele ya Waandishi wa habari wa Shirika la Magazeti ya Serikali Zanzibarleo , juu ya mikakati mbali inayochukuliwa na mkoa huo ili kupambana na mambao mbali mbali ikiwemo , magendo ya Karafuu, Madawa ya Kulevya na shuhuli mbali mbali za kijamii.

Mwandishi wa habari wa Shirika la Magazeti ya Serikali Zanzibarleo Pemba, Abdi Juma Suleiman, akimuuliza swali Mkuu wa mkoa wa Kaskazini Pemba ,jinsi walivyojipanga kudhibiti magendo ya karafuu.

Picha na Habiba Zarali - Zanzibarleo Pemba.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.