Habari za Punde

Shangani na Muembemakumbi Zan'gara Ligi ya Wilaya ya Mjini Unguja.


Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.

Timu ya Shangani na Muembe Makumbi zimeanza vyema ligi daraja la Pili Wilaya ya Mjini baada ya kushinda michezo yao ya leo kwenye uwanja wa Amaan.

Saa 10 za jioni Shangani waliichapa Gereji 2-0 kwa mabao yaliyofungwa na Abdallah Maulid dakika ya 42 na Pesto Is-haka dakika ya 45.

Saa 8 za mchana Muembe Makumbi wakaichapa Kundemba bao 1-0 kwa bao pekee lililofungwa na Ame Ibrahim Mohammed dakika ya 76.

Ligi hiyo itaendelea tena kesho kwa kupigwa michezo miwili katika uwanja wa Amaan.

Saa 8:00 za mchana El hilali dhidi ya Kijangwani na saa 10:00 za jioni Gulioni City dhidi ya Raskazone.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.