Habari za Punde

Makamu wa Rais mama Samia awasili Kilimanjaro

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amewasili mkoani Kilimanjaro na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Anna Mghwira pamoja na Viongozi wengine wa Chama na Serikali.
Makamu wa Rais anatazamiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi  wa Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani ambayo Kitaifa yanafanyika mkoani Kilimanjaro kesho Oktoba 16, 2017.

Kauli mbiu ya mwaka huu ni " Zuia Ajali-Tii Sheria Okoa Maisha"

Ufunguzi huo utafanyika katika Uwanja wa Mashujaa uliopo katika Manispaa ya mji wa Moshi.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Anna Mghwira mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa KIA ambapo anatazamiwa kuwa mgeni rasmi katika Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Anna Mghwira mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa KIA ambapo anatazamiwa kuwa mgeni rasmi katika Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.