Habari za Punde

Mashimo ya mchanga kisiwa cha Uzi kama bao la kete







• Maji ya bahari yanyemelea kukimeza kisiwa hicho.
• Wananchi wataka ziara ya viongozi wakaojinee 

KATIKA ziara tuliyoifanya jana Oktoba 21, 2017 waandishi wa habari wanne kutoka vyombo mbalimbali katika kijiji cha Uzi Mkoa wa Kusini Unguja, tulibaini uharibifu mkubwa wa mazingira unaotokana na uchimbaji ovyo wa mchanga.

Uchimbaji huo wa mchanga ulioshamiri sasa baada ya kujitokeza mahitaji makubwa ya rasilimali hiyo kufuatia udhubiti wa Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo a Uvuvi, unawanyima usingizi wananchi wa Uzi, huku wakidai hali inakuwa mbaya zaidi kwa kuwa hakuna hatua yoyote inayochukuliwa licha ya taarifa wanazozitoa kwa uongozi wa shehia. 

Baharini nako kuna tishio kwani mashimo zaidi ya 65 yanayochimbwa mchanga yako mita chache kutoka ufukweni na tayari miti mingi ikiwemo minazi na miembe imeanguka na mingine imeshainama kama inayorukuu, hali inayotishia maji ya bahari kukivamia kisiwa cha Uzi katika miaka michache ikiwa hatua za haraka kunusuru hali hiyo hazitachukuliwa.

Shida nyengine inayowaliza ni ukosefu wa maji ya bomba, ambapo tulibaini mifereji mingi kila kona ya kijiji hicho ikiwa mikavu huku mingine ikiwa imekatwa kabisa.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.