Habari za Punde

Waziri Profesa Jumanne Maghembe Afurahia Bidhaa za Kampuni ya Ivori ya Iringa.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe akiwa ameshika bidhaa za kampuni ya Ivori Iringa  ambazo ni chocolate na pipi za maziwa alipotembelea banda la kampuni hiyo katika maonyesho ya utalii wa kanda ya nyanda za juu kusini yalifanyikia katika mkoa wa Iringa viwanja vya kanisa la kikatoliki la parokia ya kihesa maarufu kama uwanja wa kichangani.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe akiwa  sambamba na mkuu wa mkoa wa iringa bi Amina Masenza walipotembelea banda la kampuni ya Ivori Iringa katika maonyesho ya utalii wa kanda ya nyanda za juu kusini yalifanyikia katika mkoa wa Iringa viwanja vya kanisa la kikatoliki la parokia ya kihesa maarufu kama uwanja wa kichangani.
 Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akiomuonyesha waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe baadhi ya bidhaa za kampuni ya Ivori Iringa katika maonyesho ya utalii wa kanda ya nyanda za juu kusini yalifanyikia katika mkoa wa Iringa viwanja vya kanisa la kikatoliki la parokia ya kihesa maarufu kama uwanja wa kichangani.


Na Fredy Mgunda,Iringa.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe amezipongeza bidha zinazozalishwa na kampuni ya Ivori Iringa (I.F.B) iliyopo mkoani Iringa kuwa ni dhaa zenyeubora unatakiwa kwa afya ya mwanadamu hivyo kuwataka wananchi kuendelea kuzitumia ili kuvikuza viwanda vyetu vya ndani vinavoyetengeneza bidhaa bora kama za kampuni hii.

Akizungumza wakati wa kufungua maonyesho ya utalii wa kanda ya nyanda za juu kusini katika viwanja vya kichangani mkoani Irirnga Prof.Maghembe amekuwa akitumia bidhaa za Ivori mara kwa mara bado anazipenda kutokana na ubora wake.

“Hata akija mtu kutoka nje ya nchi hawezi amini kama bidhaa kama hizi za Ivori zinatengezwa Iringa Tanzania maana zimekuwa na ubora unastahili ndio maana leo kwenye maonyesho haya nimetembelea kwenye banda hili na kukuta bidhaa mchanganyiko wa kampuni ya Ivori Iringa (I.F.B)”alisema Prof. maghembe

Aidha Prof. maghembe aliwaomba viongozi wa mkoa wa Iringa na watanzania kwa ujumla kuendelea kuzitumia bidhaa hizo kwa kuzimia kwa lengo loa kuinua uchumi wa wazalendo hasa hivi viwanda wa wananchi wazawa tuvikumbatie ili kuendelea kutoa ajira kwa wananchi wengine.

“Nimeonja hizi chocolate za kampuni ya Ivori Iringa kwa kweli kama zile ambazo huwa nazinunua nikiwa ulaya au marekani jamani watanzania wenzangu tuendelee kutumia bidhaa bora zinazotengenezwa na kampuni zetu za kizalendo” alisema prof. maghembe.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza alisema kuwa kampuni ya Ivori Iringa imekuwa ikizalisha bidhaa bora na zenye viwango vya kimataifa ndio maana zimekuwa zikipendwa na watu wengi.

“Ukitembea karibia maeneo yote hapa nchi Tanzania huwezi kuzikosa bidhaa za Ivori Iringa kutokana na ubora wake hivyo wanasii tu waongeze wigo wa soko la bidhaa zao bila woga maana zinaubora unaotakiwa” alisema Masenza

Lakini nikukumshe tu mnamo tarehe 16 mwezi wa nne mwaka 2016 kampuni ya Ivori Iringa ilitoa angalizo kwa watumiaji wa bidhaa zao kwa kuwa kumekuwa chocolate zinazofanana na chocolate za kampuni hiyo.

Kama wewe ni mmoja kati ya watu ambao umekua ukikutana na Chocolate inayotoka nje ya Nchi yenye nembo inayofananishwa na Chocolate ya Ivori Iringa ukahisi labda wamebadilisha muonekano wa nembo yao sasa Uongozi wa Kampuni ya IVORI IRINGA inayo majibu yake kwenye hizi sentensi 5 na inabidi uzingatie pia unapoenda dukani kununua.

1-Kuhakikisha kila bidhaa unayonunua ya IVORI ina Nembo Halisi ya IVORI yenye Herufi I mwanzoni na herufi I  mwishoni.

isomeke IVORI CHOCOLATE na Sio IVORY CHOCOLATE

2-Bidhaa zetu zote zinatengenezwa TANZANIA,Tunajivunia Uzalendo wetu na ndio maana bidhaa zetu zote ni MADE IN TANZANIA .

3-Hakikisha kila  Chocolate yetu unayoinunua ina Rangi ya kahawia ndani ya pakiti yake ikiwa na Ladha tamu ya maziwa ikitegenezewa na COCOA Halisi inayolimwa na Wakulima Nchini TANZANIA

4-Rangi ya kifungashio chakeni ya Njano iliyochanganywa na Rangi ya Zambarau.

5-Gharama zetu Elekezi ni Shilingi 1000 kwa Gram 40 na Shilingi 500 kwa Gram 20 na hatuna ujazo unaozid gram 40.

Iwapo kuna utofauti wa Bidhaa unayoiona na kuitilia shaka kampuni ya IVORI wanaomba sana uwasiliane nao kwa sababu  inabidi uwe Mjanja ili Usidanganyike Kununua Bidhaa Feki,Nunua Bidhaa Orijino Za Ivori Iringa, Epuka Kutapeliwa.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.