Habari za Punde

PBZ Yaibuka Mshindi wa Pili PBZ Mkombozi Cup 2017 Baada ya Kufungwa na Timu ya FFU. Kwa Bao 2--0.

Kikosi cha Timu ya PBZ Zanzibar kilichotowa upinzani wakati wa mchezo wao wa Fainali ya Kombe la PBZ Mkombozi Cup 2017 mchezo uliofanyika uwanja wa Amaan Zanzibar, Michuano hiyo imeandaliwa na Benki ya Watu wa Zanzibar Ltd. na kushirikisha Timu 14 za Mashirika na Serikali kuunda udugu katika Sekta ya Michezo Zanzibar kupitia Taasisi zao .
Michuano hiyo itakuwa endelevu kila mwaka.
Kikosi cha Timu ya PBZ wakiwa na Viongozi wao baada ya kukabidhiwa Kombe la Mshindi wa Pili wa Michuano ya PBZ Mkombozi Cup 2017. mchezo huo umefanyika uwanja wa Amaan Zanzibar. 

Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utalii Utamaduni nas Michezo Omar Hassan King akisalimiana na wachezaji wa Timu ya PBZ kabla ya kuaza kwa mchezo wao wa Fainali ya Kombe la PBZ Mkombozi CUP 2017.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utalii Utamaduni nas Michezo Omar Hassan King akisalimiana na wachezaji wa Timu ya FFU kabla ya kuaza kwa mchezo wao wa Fainali ya Kombe la FFU Mkombozi CUP 2017.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utalii Utamaduni na Michezo Omar Hassan King akisalimiana na Waamuzi wa Mchezo huo wa Fainali ya PBZ Mkombozi Cup 2017. akimsalimia muamuzi wa mchezo huo Abubakar Khatib ameweza kuumudu mchezo huo kwa uchezeshaji wake bila ya upendeleo kwa upande wowote wakati wa mchezo huo.Wakwanza Rashid Ramadhani, Suleiman Zuhuri,Abubakary Khatib na Hija Haji. 

Kikosi cha Timu ya FFU kilichotowa Ubingwa wa Michuano ya PBZ Mkombozi Cup 2017 kwa kuifunga Timu ya PBZ muandalizi wa michuano hiyo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.