Habari za Punde

Azam yalala 1-0 dhidi ya URA ya Uganda


Na Salum Vuai, 


AZAM FC  imeshindwa kuendeleza wimbi la ushindi kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi baada ya kufungwa 1-0 na URA ya Uganda katika mchezo wa Kundi A jioni ya leo Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Bao pekee lililoizamisha Azam FC iliyokuwa na rekodi ya kutoruhusu nyavu zake kuguswa kwa mechi saba tangu msimu uliopita, limefungwa na Nicholaus Kagaba.

Katika mchezo huo, Azam FC ilimaliza pungufu baada ya winga wake Mghana, Enock Atta-Agyei kutolewa kwa kadi nyekundu kwa mchezo usio wa kiungwana.Mchezo uliotangulia wa Kundi B, Singida United iliendeleza wimbi la ushindi baada ya kuichapa Mlandege FC 3-0, mabao ya Danny Usengimana kwa penalti, K. Mwambungu na L.Mbia.


Matokeo hayo yanamaanisha Singida United imetingia Nusu Fainali ya michuano hiyo. 

Mechi ya mwisho leo inafuatia Saa 2:15 usiku hii kati ya Yanga SC na Taifa ya Jang’ombe.  

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.