Waziri wa
Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Juma Homera (katikati) akizungumza na watumishi wa
THBUB (hawapo pichani) wakati wa ziara ya kuitembelea ofisi hiyo makao makuu
Dodoma, kulia ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Zainabu Katimba na
Mwenyekiti wa THBUB, Mhe. Jaji Mathew Mwaimu (Mst) (wa kwanza kushoto). Picha
na THBUB.
NA
MWASHAMBA JUMA, THBUB
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora
(THBUB) imetakiwa kuwa sehemu ya kulinda amani ya nchi ili kuipa Tanzania sura
nzuri ndani na nje ya mipaka yake.
Rai hiyo imetolewa na Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Juma Homera alipozungumza
na Viongozi na watumishi wa tume hiyo wakati wa ziara yake katika ofisi za THBUB
Makao Makuu, Jijini Dodoma, Novemba 26, 2025.
Mhe. Homera ameeleza kuwa THBUB imepewa mamlaka makubwa na Katiba ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania ya kuhakikisha haki za binadamu zinalindwa nakuhifadhiwa
nchini Tanzania ili amani iliyokuwepo enzi na enzi iendelee kudumishwa.
“Tumekuwa kimbilo la wengi sababu ya amani tuliyo nayo nchini. Hili ni tunda
tunalojivunia, ninyi THBUB ni jukumu lenu kuwaelimisha wananchi kuhusu haki na
wajibu pamoja na umuhimu wa kuilinda amani iliyopo" Alieleza Mhe. Homera
Aidha, Mhe. Dkt. Homera ameipongeza THBUB kwa namna inavyotekeleza majukumu
yake kwa weledi na kuahidi kutoa ushirikiano katika kipindi chote
atakachotumika akiwa Waziri wa Katiba na Sheria kwa maslahi mapana ya Taifa.
Akizungumza katika hafla hiyo wakati akimkaribisha Mhe. Waziri, Naibu Waziri wa
Katiba na Sheria, Mhe. Zainabu Katimba ametoa wito kwa THBUB wakiwa
wanatekeleza majukumu yao, kuwakumbusha wananchi kuwa haki na wajibu ni mambo
yanayokwenda sambamba na kuwa haki za binadamu zina wigo mpana lakini zina
mipaka pia.
“Kila mtu ana wajibu wa kuhakikisha anapo furahia haki zake za msingi haiingilii
haki za mwingine” Alisema Mhe. Katimba.
Naye Mwenyekiti wa THBUB, Mhe. Jaji Mathew Mwaimu (Mst) akitoa taarifa ya
utekelezaji wa tume hiyo, ameishukuru Wizara ya Katiba na Sheria kwa namna
inavyoendelea kushirikiana na Tume kwa kuiwezesha kutekeleza majukumu yake na
kuahidi kuendeleza ushirikiano uliopo.
1. Waziri wa
Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Juma Homera (katikati) akizungumza na watumishi wa
THBUB wakati wa ziara ya kuitembelea ofisi hiyo makao makuu Dodoma, Novemba 26,
2025.
Naibu Waziri
wa Katiba na Sheria, Mhe. Zainabu Katimba (kulia)akizungumza na watumishi wa
THBUB (hawapo pichani) wakati wa ziara yake na Waziri wa Wizara hiyo kwa THBUB
(katikati) wa Kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa THBUB, Mhe. Jaji Mathew Mwaimu
(Mst).
. Waziri wa
Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Juma Homera (katikati aliyekaa) akiwa katika picha
ya pamoja na watumishi wa THBUB alipowatembelea Makao Makuu jijini Dodoma,
Novemba 26, 2025. Wapili kushoto (aliyekaa) ni Naibu Waziri Mhe. Zainabu
Katimba na wapili kulia (aliye kaa) ni Mwenyekiti wa THBUB, Mhe. Jaji Mathew
Mwaimu (Mst). Picha na THBUB.
0 Comments