Na Munir Shemweta, Mtwara
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Leonard Akwilapo amezitaka taasisi za umma kuhakikisha zinalinda mipaka ya maeneo yake ili kuepuka uvamizi unaoweza kuzalisha migogoro ya ardhi nchini.
Mhe Dkt Akwilapo ametoa rai hiyo mapema leo tarehe 27 Novemba 2025 mkoani Mtwara alipozungumza wakati wa kikao na uongozi wa mkoa katika ziara yake mkoani humo.
"Tuhakikishe tunazuia uvamizi ili kuepuka migogoro ya baadaye hii itatusaidia sana kama wizara kushughulika na masuala ya jamii, migogoro ya ardhi ni mingi" amesema
Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Mtwara Bw. Fredrick Mrema ameeleza katika kikao hicho kuwa, mkoa wa Mtwara kwa sasa unakabiliwa na migogoro mikubwa saba ya ardhi katika maeneo mbalimbali mkoani humo.
Ameitaja baadhi ya migogoro hiyo kuwa, ni ile inayohusisha wananchi wa Mbae na Mayanga na jeshi la wananchi, mgogoro wa wananchi wa eneo la uwanja wa ndege-Mngamba na halmashauri ya mtwara mikindani pamoja na ule wa wananchi wa kijiii cha Nakada kata ya Katere na mwekezaji kampuni ya Sugar-Tanzania.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ameuahidi uongozi wa mkoa wa Mtwara kuunda timu maalum kutoka makao makuu ya wizara kwenda mkoani humo kushughukia migogoro hiyo ya ardhi.
Ameeleza kuwa, kwa sasa Wizara yake imejipanga vyema kukabiliana na migogoro ya ardhi nchini kwa lengo la kuwaacha wananchi na furaha.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Leonard Akwilapo (Kushoto) akipokea taarifa ya migogoro ya ardhi kutoka kwa Katibu Tawala wa mkoa wa Mtwara CPA (T) Bahati Geuzye wakati wa ziara yake mkoani humo tarehe 27 Novemba 2025.
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
0 Comments