Habari za Punde

MAKAMU WA RAIS AKIWASILI NCHINI ANGOLA KUMWAKILISHA RAIS DKT. SAMIA KATIKA MKUTANO WA AFRIKA NA UMOJA WA ULAYA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Quatro de Fevereiro, Jijini Luanda nchini Angola leo tarehe 23 Novemba 2025. Makamu wa Rais, anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa 7 wa Kilele wa Viongozi wa Umoja wa Afrika na Umoja wa Ulaya (AU-EU Summit), utakaofanyika tarehe 24 na 25 Novemba 2025 Jijini Luanda.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Ndani wa Jamhuri ya Angola Mhe. Manuel Homem wakati alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Quatro de Fevereiro, Jijini Luanda nchini Angola leo tarehe 23 Novemba 2025. Makamu wa Rais, anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa 7 wa Kilele wa Viongozi wa Umoja wa Afrika na Umoja wa Ulaya (AU-EU Summit), utakaofanyika tarehe 24 na 25 Novemba 2025 Jijini Luanda.

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.