Na.Omar Abdallah Wizara ya Afya.
JUMLA ya wanafunzi 167 kati ya wanafunzi 1070 waliofanyiwa uchunguzi wa macho wamepatiwa miwani baada ya kubainika kuwa na matatizo mbali mbali yakiwemo uwoni hafifu hali inayopelekea usumbufu katika masomo yao.
Akizungumza katika hafla ya kukabidhi miwani kwa wanafunzi wa shule ya Mtule, Uroa na Hasnuu Makme Mkoa Kusini Unguja Mratibu wa huduma za Macho Wizara ya Afya Zanzibar Dkt Fatma Juma Omar amaesema katika uchunguzi waliofanyiwa wanafunzi hao mwezi wa septemba mwaka huu na kuwabaini wanafunzi wapatao 167 kuwa na changamoto ya uoni na kufanikisha kuwapatiwa miwani na wengine kuwafuatilia zaidi kimatibabu.
Amesesma hatua hiyo ni sehemu ya jitihada za Srikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara ya Afya ya kuhakikisha kila mtoto kupata haki ya kuona vizur ili maendeleo yao ya elimu yaweze kufanikiwa.
Amesema wataalamu wa Afya wataendelea kuweka mkazo zaidi katika kutoa elimu, kuwafanyia uchunguzi wa matibabu ya macho ili kuhakukisha hakuna mtoto anaekosa fursa ya kuona vyema na kufikia ndoto zake za kupata elimu.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa Taasisi Charity Vision Tanzania Mariyam Bijima amesema katika kuimarisha Afya ya macho kwa wanafunzi wameona ipo haja kwa Taasisi yao kwa kushirikina na Wizara ya Afya kuwafanyia uchunguzi na kuwapatia miwani wanafunzi wa Skuli tofauti ili waweze kusoma kwa ufanisi.
Amesema wanampango wa kuwafanyia uchunguzi wanafunzi wa Skuli nyengine kupitia muongozo wa Wizara Afya kwa kutambua mahitaji ambayo wanafunzi watakuwa na matatizo ya macho na watafanikisha kuwapatia miwani sambamba na kufanyiwa uchunguzi na matibabu.
Nae Mwalimu kutoka Skuli ya Hasnuu Makame Vuai Makame Kitwana amesifu jitihada za Serikali kupitia Wizara ya Afya na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kwa kushirikiana na Taasisi mbali mbali ikiwemo Charity Vision ya Tanzania kwa kuwapatia msaada huo wa kuwapima na kuwapatia miwani kwa wanafunzi ambao utasaidia kwa kiasi kikubwa kuimarisha Afya zao na kusoma kwa ufanisi.
Amesema hatua hiyo ya kuwapatia Miwani wanafunzi hao utasaidia kwa kiasi kikubwa kuondokana na changamoto ya uwoni hafifu wakati wa kusoma na kufanikisha kuondokana na tatizo hilo.
Nae Afisa mwandamizi wa Elimu Mjumuishi na stadi za Maisha Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Hafidh Saleh ameishukuru Taasisi ya Charity Visio kwa msaada huo ambao utasaidia kuondokana na na tatizo la uwoni kwa wanafunzi na kuwataka wazidi kutoa msaada huo kwa Skuli nyengine ili kukabilina na hali hiyo.
Mwanafunzi wa Skuli ya Hasnuu Makame, Salum Suleiman Lusangija ameishukuru Taasisi hiyo kupitia Wizara ya Afya kuwapatia Miwani ambazo zitawasaidia kwa kiasi kikubwa katika masomo yao ambapo kabla kupata miwani changamoto kubwa ilikuwa katika kujisomea wakiwepo maskulini n ahata majumbani.

No comments:
Post a Comment