Habari za Punde

Inna lilah wainna ilayhi rajiun. Kiongozi Mwandamizi wa Jumuiya ya Ismailiya Alhajj Sherali Mohammedali Champsi

Makamu wa  Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Hemed Suleiman Abdulla amejumuika na Viongozi mbali mbali, wanafamilia, ndugu, jamaa na marafiki wakiongozwa na Alhajj Dkt. Hussein Ali Mwinyi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi katika Swala na Dua ya kumuombea Kiongozi Mwandamizi wa Jumuiya ya Ismailiya Alhajj Sherali Mohammedali Champsi iliyofanyika  katika msikiti wa Ijumaa Malindi Zanzibar.

Inna lilah wainna ilayhi rajiun. 

Imetolewa na Kitengo cha Habari (OMPR )

Tarehe 15.11.2025

Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Hassan Othman Ngwali akisoma dua baada ya kumalizika kwa Sala ya Maiti kumuombea Kiongozi Mwandamizi wa Jumuiya ya Ismailiya Alhajj Sherali Mohammedali Champsi iliyofanyika  katika msikiti wa Ijumaa Malindi  Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar.

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.