Habari za Punde

MSITUMIE MITANDAO YA KIJAMII KUFANYA MAKOSA YA JINAI

Jamii imeaswa kuacha tabia ya kutumia mitandao ya kijamii kuwaumiza na kuwadhalilisha watu wengine, kufanya hivyo ni uvunja haki za watu na kinyume na sheria za nchi.

Akizungumza katika mafunzo ya kuwajengea uwezo Watendaji wa Madawati ya Jinsia na watoto, leo Novemba 13, 2025 katika Chuo cha Polisi Zanzibar Wakili na Mwanasheria wa Jeshi la Polisi Kamisheni ya Polisi Zanzibar, Mkaguzi wa Polisi (INSP) SADIKI ALI SULTAN amesema  kumtisha, kumsumbua, kumshurutisha au kumuumiza kihisia mtu kwa kutumia mitandao ni kinyume na kifungu cha 23 (1) cha Sheria ya makosa ya Kimtandao, ambapo adhabu yake ni faini isiyopungua milioni tano au kifungo kisichopungua miaka mitatu au vyote kwa pamoja.

Mtendaji wa Dawati la jinsia na watoto kutoka Makao Makuu ya Polisi Stafu Sajenti MAKAME KHATIB MAKAME na Afisa hifadhi kitengo cha Mtoto kutoka Idara ya Ustawi wa Jamii FATMA MAULID ni miongoni mwa washiriki wa mafunzo ya namna kushughulikia makosa ya udhalilishaji wa kijinsia na watoto wamesema mafunzo hayo yamewajenga kushughulikia kesi za udhalilishaji kwa ufanisi.

Kitengo cha Habari,

Makao Makuu ya Polisi,

Kamisheini ya Zanzibar

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.