Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na Marais Wastaafu wa Zanzibar (kulia kwa Rais) Rais Mstaafu wa Zanzibar Mhe.Dkt.Amani Abeid Karume na (kushoto kwa Rais) Rais Mstaafu wa Zanzibar Mhe.Dkt.Ali Mohammed Shein.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amekutana na Marais Wastaafu wa Zanzibar, Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein wa Awamu ya Saba na Mhe. Amani Abeid Karume wa Awamu ya Sita, Ikulu Zanzibar tarehe 08 Novemba 2025.
Marais hao wastaafu wamemtembelea Rais Dkt. Mwinyi kwa lengo la kumpongeza kwa ushindi wa kishindo alioupata, pamoja na kupongeza hali ya amani na utulivu iliyoshuhudiwa wakati wa Uchaguzi Mkuu.


No comments:
Post a Comment