Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi Amemuapisha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla Ikulu Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amemuapisha Mhe. Hemed Suleiman Abdulla kuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.

Mhe. Hemed Suleiman Abdulla ameteuliwa kushika wadhifa huo kwa mara ya pili katika Awamu ya Nane ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Hafla ya uapisho imefanyika leo, tarehe 08 Novemba 2025, Ikulu Zanzibar, na imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo viongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, viongozi wa dini, Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama kutoka SMZ na SMT, pamoja na wanafamilia.








No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.