Habari za Punde

MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR- AKIMUWAKILISHA RAIS WA ZANZIBAR - KATIKA YAS ZANZIBAR INTERNATIONAL MARATHON....MAISARA

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akimwakilisha Dkt. Hussein Ali Mwinyi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi katika mashindano ya Yas Zanzibar International Marathon 2025 yaliyofanyika katika viwanja vya michezo Maisara Zanzibar.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akimwakilisha Dkt. Hussein Ali Mwinyi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi katika mashindano ya Yas Zanzibar International Marathon 2025 yaliyofanyika katika viwanja vya michezo Maisara Zanzibar.


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaiendeleza azma yake ya kuboresha na kuimarisha Sekta ya Michezo nchini.                                                                                                                  

Ameyasema hayo kwa niaba ya Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Zanzibar  na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi katika uzinduzi wa Mashindano ya Yas Zanzibar International Marathon yalifanyika katika Viwanja vya Michezo  Maisara Zanzibar.

Amesema Rais Dkt. Hussein Mwinyi ameahidi kuiendeleza sekta ya Michezo kwa kujengwa na kuboreshwa miundombinu ya michezo ikiwemo kujenga Viwanja mbali mbali vya michezo pamoja na ujenzi wa Mji wa michezo unaojengwa katika kijiji cha Fumba wilaya ya Magharibi “B”  Unguja.

Mhe. Hemed amesema uwepo wa miundombinu baora ya michezo kutaipelekea nchi kupiga hatua za  kimaendeleo,  kuitangaza nchi Kitaifa na Kimataifa sambamba na wanamichezo kupata ajira ndani na nje ya nchi.

Mhe. Hemed ameyaagiza Mashirika yote ya ndani kuendelea kushirikiana na waandaaji wa Mashindano ya Zanzibar International Marathon ili yaweze kuboreka zaidi na kuwavutia wanamichezo kutoka nchi mbali mbali kuja kushiriki katika mashindano hayo.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amewasisitiza wanamichezo na wananchi kwa ujumla kuendelea kudumisha Amani na utulivu uliopo nchini sambamba na  kuendeleza umoja na ushirikiano katika kuijenga zanzibar ya maendeleo.

Kwa upande wake Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Zanzibar Mhe. Riziki Pembe Juma ameipongeza Kampuni ya Mix by Yas kwa kuendelea kuandaa mashindano hayo  yanayowakutanisha wanamichezo kutoka nchi mbali mbali jambo ambalo huwajenga wanamichezo kuwa na  umoja na mshikamano pamoja na kuongeza mapoto ya nchini kupitia Utalii wa Michezo.

Waziri Pembe amesema Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo iko tayari kutoa ushirikiano kwa wadau mbali mbali wa michezo katika kukuza na kuimarisha sekta ya hio nchini.

Nae Afisa Mtendaji Mkuu Kutoka Kampuni ya Mix By Yas  Tanzania ambao ndio wadhamini wakuu wa mashindano hayo Bibi Angelica Peshe amesema Kampuni hio imekuwa ikifanya kazi kwa karibu sana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa lengo la kuhakikisha inaunga mkono jitihahada zinazofanywa na serikali hasa katika kufungua fursa za kifedha na kukuza uchumi nchini.

Angelica amesema Kampuni ya Mix by Yas kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mji mkongwe Zanzibar,  Mamlaka ya Mapato Zanzibar (ZRA) na Mamlaka ya Mapato Tanzani(TRA) imeimarisha Mfumo wa kidijitali wa ukusanyaji wa  mapato kwa lengo la kuongeza ufanisi wa ufanyaji kazi, kuzibiti mapato ya serikali  na kupunguza changamoto ya foleni kwa wananchi wanaofuata huduma katika Taasis hizo.

Amefahamisha kuwa Kampuni ya Mix by Yass itaendela kutoa mchango wake kupitia Sekta ya Utalii na Michezo ili kuhakikisha sekta hizo  zinazidi kukua na kuimarika kupitia Utalii wa Michezo jambo ambalo litatoa faida chanya kwao na kwa Wazanzibari kwa ujumla.

Mwenyekiti wa Mashindano ya Zanzibar International Marathon ndugu Hassan Mussa Ibrahim ameishukuru kampuni ya Yas kwa kuendelea kudhamini mashindano hayo kwa mwaka wa Nne mfululizo jambo linaloakisi dhamira yao ya kuunga mkono    jitihada mbali mbali zinazofanywa na Serikali katika kukuza sekta ya michezo hasa katika kuimarisha  Utalii wa Michezo.

Katika mashindano hayo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amewazawadia mfano wa hundi  yenye fedha taslim shilingi milioni tatu (3 ) kwa washindi wa mbio za kilomita 21 na shilingi milioni mbili  kwa washindi wa mbio za kilomita 10 kwa wanawake na wanaume.

Imetolewa na Kitengo cha Habari ( OMPR )

Leo tarehe  23. 11. 2025. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.