Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Rais Mstaafu Wa Awamu ya Nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Mhitimu wa Shahada ya Awali ya Sheria ambaye alivunja rekodi iliyodumu miaka 32 kwa kupata Daraja la Kwanza katika Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (The Law School of Tanzania), rekodi iliyokuwa inashikiliwa na Profesa wa sheria UDSM Prof. Hamudi Majamba.
Bi Mary Barney Laseko anakuwa mwanamke wa pili kupata daraja la kwanza kutoka Law School of Tanzania, wa kwanza akiwa Katibu Mkuu wa `CCM Dkt. Asha-Rose Migiro.
Hii imetokea leo wakati wa Mahafali ya 55 (Duru la Tatu) ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam yaliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam.
Kwenye Mahafali hayo Dkt Kikwete ametunuku Shahada na Stashahada kwa jumla ya wahitimu 2,452 ambapo 1,386 ama asilimia 56.6 ni wanawake. Picha na Issa Michuzi.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Rais Mstaafu Wa Awamu ya Nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Bi. Mary Barney Isaac Laseko Mhitimu wa Shahada ya Awali ya Sheria ambaye amevunja rekodi iliyodumu miaka 32 kwa kupata Daraja la Kwanza katika Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (The Law School of Tanzania), rekodi iliyokuwa inashikiliwa na Profesa wa sheria UDSM Prof. Hamudi Majamba. Pemebni ni wazazi wake Bw. Barney Isaac Laseko na Mama LAseko,
Bi Mary Barney Laseko anakuwa mwanamke wa pili kupata daraja la kwanza kutoka Law School of Tanzania, wa kwanza akiwa Katibu Mkuu wa `CCM Dkt. Asha-Rose Migiro.
Hii imetokea leo wakati wa Mahafali ya 55 (Duru la Tatu) ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam yaliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam.
Kwenye Mahafali hayo Dkt Kikwete ametunuku Shahada na Stashahada kwa jumla ya wahitimu 2,452 ambapo 1,386 ama asilimia 56.6 ni wanawake. Picha na Issa Michuzi.

No comments:
Post a Comment