Habari za Punde

Waziri wa Afya aendelea na ziara yake Hospitali ya Rufaa Mnazi mmoja

  Waziri wa Afya wa Zanzibar Hamad Rashid Mohamed akimsikiliza mmoja ya wauguzi wa kitengo cha Watoto Hospial ya Mnazi mmoja mara baada ya kufanya ziara ya kukagua Wodi ya watoto kufahamu changamoto zinazoikabili wodi hiyo
Waziri wa Afya wa Zanzibara Hamad Rashid Mohamed akimbeba mtoto Abdulkarim Khamis Abdallah ambaye anaugua maradhi ya moyo katika chumba cha matibabu ya maradhi hayo Hospital ya Mnazi mmoja ambapo Madaktari wa maradhi ya Moyo kutoka nchini Isarael na Kanada wameweka kambi ya siku tatu ya matibabu ya watoto wanaosumbuliwa na maradhi hayo. Picha na Abdallah Omar-Maelezo Zanzibar

 Waziri wa Afya wa Zanzibara Hamad Rashid Mohamed akiwashukuru Madaktari bingwa wa maradhi ya Moyo kutoka nchini Isarael na Kanada kwa kuweka kambi ya siku tatu ya matibabu ya watoto wenye maradhi ya moyo katika chumba cha matibabu ya maradhi hayo Hospital ya Mnazi mmoja. Kulia ni Mratibu wa matibabu hayo Zanzibar Dkt. Omar Mohamed. Picha na Abdallah Omar-Maelezo Zanzibar

 Waziri wa Afya wa Zanzibara Hamad Rashid Mohamed akisalimiana na Wazazi wa Watoto wenye maradhi ya moyo katika wodi ya watoto Hospital ya Mnazi mmoja.Picha na Abdallah Omar-Maelezo Zanzibar

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.