Habari za Punde

Waziri wa Afya azindua bodi ya ushauri ya wakala wa chakula dawa na vipodozi Zanzibar (ZFDA).

 Waziri wa Afya Zanzibar Hamad Rashid Mohamed akitia saini kitabu cha wageni baada ya kufika ofisini hapo Mombasa kwaajili ya kuzindua bodi ya ushauri ya wakala wa chakula dawa na vipodozi Zanzibar (ZFDA).
 Mkurugenzi wa Wakala wa chakula dawa na vipodozi Burhani Othmani Simai akizungumza machache na kumkaribisha M\Kiti mpya wa Bodi ya ushauri ya wakala wa chakula dawa na vipodozi Zanzibar (ZFDA).
  Mwenyekiti Mpya wa Bodi ya  ushauri ya wakala wa chakula dawa na vipodozi Zanzibar (ZFDA) Mayasa Ali Salum akizungumza machache katika uzinduzi wa bodi hiyo.
  Waziri wa Afya Zanzibar Hamad Rashid Mohamed akiizundua  bodi ya ushauri ya wakala wa chakula dawa na vipodozi Zanzibar (ZFDA) katika ukumbi wa ofisi hizo Mombasa Mjini Zanzibar.
 Baadhi ya wafanya kazi wa Bodi ya ushauri ya wakala wa chakula dawa na vipodozi Zanzibar (ZFDA) waliohudhuria uzinduzi wa Bodi hiyo.
 Waziri wa Afya Zanzibar Hamad Rashid Mohamed akimkabidhi Vitendea kazi Mwenyekiti wa Bodi ya ushauri ya wakala wa chakula dawa na vipodozi Zanzibar (ZFDA) Mayasa Ali Salum.
 Waziri wa Afya Zanzibar Hamad Rashid Mohamed katikati waliokaa akiwa katika picha ya pamoja na Bodi mpya ya ushauri ya wakala wa chakula dawa na vipodozi Zanzibar (ZFDA).
Waziri wa Afya Zanzibar Hamad Rashid Mohamed katikati waliokaa akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Bodi  ya ZDFA (Picha na Abdalla Omar Maelezo – Zanzibar).

Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar 21.03.2018
Wakala wa Chakula na Dawa Zanzibar ZFDA umetakiwa kuendeleza juhudi za kuleta ufanisi katika majukumu yake ili kuzidi kujenga imani na kupata sifa za kimataifa.
Sifa hizo zitaepelekea Wadau kutoka nje ya Zanzibar kuja kujifunza namna Wakala huo unavyofanya kazi za kulinda na kuimarisha afya ya jamii kwa maslahi mapana ya taifa.
Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed ameyasema hayo wakati akizindua Bodi ya Ushauri wa Wakala huo  katika ofisi za ZFDA Mombasa mjini Zanzibar.
Amesema kinachohitajika katika Wakala huo ni kujiamini na kusimamia sheria ambazo zimewekwa kwa ajili ya kumlinda mtumiaji.
Amewasisitiza Watendaji wa ZFDA kuzikamata na kuziangamiza bidhaa zote zisizokidhi viwango hadaharani na kwa mujibu wa Idadi waliyoitangaza ili kuondoa tuhuma ambazo baadhi ya wananchi huzitoa.
amesema yapo madai kwamba wanakamata bidhaa lakini wanapoziteketeza  wananchi hawapewi taarifa kamili ya ueteketezwaji huo hivyo akasisitiza taarifa kutolewa kwa uzito wake.
Amewanasihi kuwa wanakabiliwa na majukumu kubwa ya kuhakikisha Vyakula, Dawa na Vipodozi vinavyoingizwa vinakuwa katika hali ya ubora ili kuepuka jukumu kwa maslahi yao ya hapa duniani na kesho mbele ya Mungu.
“Mnajukumu kubwa mbele ya Mungu mkiruhusu mali na bidhaa mbovu mtaenda kuwajibika siku ya malipo”aliwanasihi Waziri wa Afya.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya ZFDA Mayasa Ally Salim amesema utaratibu wa udhibiti unafanywa kupitia idara nne za wakala zikiwemo Idara ya usalama wa chakula, Idara ya Dawa Vipondozi na bidhaa za tiba, Idara ya Huduma za maabara na Idara ya human a wakala.
Amesema kazi kubwa ya ZFDA ni kulinda na kuimarisha afya ya jamii kwa kusimamia udhibiti wa bidhaa za chakula, Dawa, Vipodozi, Vifaa Tiba na Vitendanishi kupitia usajili, ukaguzi na uchunguzi wa kimaabara.
Awali akimkaribisha mgeni Rasmi Mkurugenzi wa ZFDA Burhan Othman  Simai alimuhakikishia kuwa Idara yake ipo tayari kufua kila ushauri ambao utazidikuleta ufanisi kwa kazi yake.
Wakati huo huo ZFDA ilipokea Msaada wa Gari mbili zenye thamani ya Shilingi Milioni 150  kutoka Mfuko wa Kimatifa wa Global Foundation ambazo zitatumika kwa ajili ya kufuatilia usajili,ukaguzi na uchunguzi wa kimaabara kwa Unguja na Pemba.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.