Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Mhe. Rashid Ali Juma amekutana na wawezekaji kutoka Namibia waliokuja kuangalia uwezekano wa uwekejaji katika sekta ya uvuvi, wanataka kuwekeza kwenye uvuvi wa samaki wadogo wadogo na tayari washawekeza nchi nyingi iliwemo Kenya.
Akitoa maelezo mafupi mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Uvuvi Nd. Mussa Aboud Jumbe alimueleza Mh. Waziri kuwa tayari washawapatia wawekejaji hao taarifa za awali walizozihitaji na mazungumzo yapo katika hatua nzuri.
Pia Nd. Mussa alimueleza Mh. Rashid kuwa tayari wawekezaji hao wanashirikiana na Kampuni ya Uvuvi Zanzibar (ZAFICO), ili ZAFICO iweze kusimamia shughuli zote watakazo endesha wawekejaji hao.
Kwa upande wake Mh. Rashid amewakaribisha wawekezaji hao na kuwaahidi kupata kila aina ya mashirikiano watakayo hitaji na kuwataka kufika ofisini kwake pale watakapoona panahitajika, pia aliwataka watendaji wa wizara kilimo kuhakikisha wanawapa kila aina ya mashirikiano watakayo hitaji wawekezaji hao
No comments:
Post a Comment