Habari za Punde

Zidane:Najivunia kuwa sehemu ya Mafanikio ya Real Madrid

Zinedine Zidane amesema anajivunia kuweka historia na Real Madrid baada ya kunyakua taji la ligi ya mabingwa dhidi ya Liverpool siku ya Jumamosi.
Real Madrid ilishinda mabao 3-1 huku Gareth Bale akifunga magoli mawili
Real ni timu yenye mafanikio zaidi kwenye historia ya ligi ya mabingwa ikiwa na mataji 13.
Zidane alisema:''hii ni klabu ya wakongwe. Klabu hii imeshinda makombe 13 ya Ulaya nafurahi kuwa sehemu ya historia hii
Aliongeza: '' tunakwenda kufikiria kuhusu tulichokipata, kufurahia wakati huu kwanza.Ni kitu muhimu zaidi kwa sasa''.
Real Madrid ilianza na kikosi cha kwanza dhidi ya Liverpool kama walivyofanya kwenye michuano ya mwaka 2016-17Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionReal Madrid ilianza na kikosi cha kwanza dhidi ya Liverpool kama walivyofanya kwenye michuano ya mwaka 2016-17
Timu tatu pekee zimeshinda kombe la mabingwa barani Ulaya, Real ikiwa na mataji matano tangu mwaka 1956, Ajax (1971-73) na Bayern Munich (1974-76).
Hata hivyo Real ni ya kwanza tangu kubadilishwa kwa jina la michuano hiyo.
Kiungo Luka Modric anaamini itakuwa ngumu kwa timu kufikia mafanikio ya Real
''Ni jambo la ajabu la kihistoria, aliiambia BT Sport ''Sijui kama kuna mtu atarudia hili siku za usoni.''

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.