Habari za Punde

Mkuu wa Wuilaya ya Magharibi B Unguja Awataka Wanafunzi Kuepuka na Vitendo Vya Utumiaji wa Dawa za Kulevya.

Na Takdir Ali, Maelezo Zanzibar.   25-06-2018.
Mkuu  wa Wilaya ya Magharibi “B” Kepteni Silima Haji Haji amewataka Wanafunzi kuacha kujiingiza katika vitendo viovu ikiwemo utumiaji wa Dawa za kulevya na Bangi ili kuepukana na kuharibu Maisha yao.
Amesema kitendo cha baadhi ya Wanafunzi kujiingiza katika vitendo viovu mara wanapomaliza masomo kimekuwa kikirudisha nyuma Serikali kwani lengo lake ni kuwaona wanakuwa raia wema wa kujenga nchi yao.
Akizungumza na Waalimu na Wanafunzi waliomajiliza Kidato cha sita Skuli ya Sekondari Mwanakwerekwe C amesema utumiaji wa Dawa za kulevya umekuwa ukileta athari ya kiafya na Kisaikolojia kwa vijana wanaotumia dawa za kulevya, hivyo ni vyema kuepukana na kujiingiza katika janga hilo.
Aidha amewataka Wanafunzi wa kike kuacha kujishirikisha katika vitendo hivyo kwani vinasababisha kujiingiza katika Ndoa za mapema na Mimba za umri mdogo jambo ambalo linapaswa kupigwa vita kwa hali na mali.
Mbali na hayo amewataka Wazazi kuwashajiisha Watoto wao wasome kwa bidii hasa masomo ya Sayansi ili waweze kupata vijana watakaoweza kuwasidia katika kuendesha maisha yao na taifa kwa ujumla.
Kwa upande wake Afisa elimu Sekondari Mwalimu Khalifa Rashid amesema amewapongeza Walimimu wa Skuli hiyo kwa juhudi wanazozichukuwa katika kuwafunzisha Wanafunzi na kuweza kufanya vizuri Mitihani yao ya Taifa ambapo amesema hatua hiyo imefikia wanafunzi hao kufanya vizuri katika Mitihani ya Taifa.
Amewataka waalimu kutovunjika moyo licha ya kufanya kazi katika mazingira magumu na Serikali inachukuwa juhudi za makusudi kuhakikisha matatizo hayo yanatatuka ili kuwaondoshea usumbufu Waalimu hao.
Mwalimu Mkuu wa Skuli hiyo amesema Ibrahim Kasim Saleh amesema  Waalimu wake wamekuwa wakifanya kazi katika Mazingira lakini wamekuwa wakifanya vizuri mitihani yao ya Taifa.
Hata hivyo amesema wamekuwa wakikabiliwa na matatizo mbali mbali ikiwemo Tatizo la gharama za ulipaji wa Umeme ambapo kwa mwezi wamekuwa wakilipia kiasi ya laki 4 jambo ambalo limekuwa likiwaweka katika wakati mgumu na kuomba kufungiwa Umeme wa Sola ili wapate nafuu.
Wakizungumza kwa niaba ya wenzao Mwanafunzi Yahya Omar Khalfani na Zainab Kesi Hassan wameahidi kuyafanyia kazi kwa vitendo maelekezo waliopewa na Mkuu wa Wilaya ili kuweza kufikia malengo ya Serikali na kuwa raia wema wa Taifa lao.
     Imetolewa na Idara Idara ya Habari Maelezo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.