Habari za Punde

Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zuberi Ali Maulid. Akitowa Taarifa Kwa Wajumbe, Kiti cha Mjumbe Mwakilishi wa Jimbo la Jangombe Kipo Wazi.

Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zuberi Ali Maulid akisima Taarifa rasmin kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar kuwa nafasi ya Kiti cha Uwakilishi Jimbo la Jangombe iko wazi baada ya Mjumbe wa Jimbo hilo kuvuliwa Uwanachama wake na Chama cha Mapinduzi Ndg. Abdallah Maulid Diwani.

Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe., Zuberi Ali Maulid akitowa taarifa kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi baada ya kupokea barua kutoka kwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kuhusiana na "Kufukuzwa Uanachama wa Chama cha Mapinduzi Ndg. Abdallah Maulid Diwani " Mwakilishi wa Jimbo la Jangombe Zanzibar yenye kumbukumbu Namba MVW/26/HQ3/43 ya tarehe 30 Mei,2018.

Amesema barua hiyo imeeleza kuwa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Mjini iliokutana tarehe 5 April 2018 imemfukuza uanachama Mheshimiwa Abdallah Maulid Diwani -Mwakilishi wa Jimbo la Jangombe Zanzibar chini ya Ibara ya 89(14) ya Katiba ya CCM toleo la 2017 baada ya kuthibitisha tuhuma za ukiukwaji wa Kanuni za Uongozi na Maadili za CCM.

Kufuatia uamuzi huo, Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM iliyokutana tarehe 28-29,Mei 2018, iliridhia uamuzi huo na hivyo ilimfukuza katika uongozi wa CCM  Mwakilishi huyo chini ya Ibara ya 102(21) ya Katiba ya Chama 

Amesema kutokana na maamuzi hayo na kwa mujibu wa Kifungu cha 71(1) (a) kikisomwa pamoja na kifungu cha 68(d) vya Katiba ya Zanzibar 1984, Mjumbe Mwakilishi huyo amekosa sifa ya kuwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi .Hivyo kwa mujibu wa kifungu cha 71(2) cha Katiba ya Zanzibar ya 1984, naomba kutoa taarifa rasmi kwamba Kiti cha Mjumbe Mwakilishi cha Jimbo la Jangombe kipo wapi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.