Habari za Punde

Wananchi na Watoto Kijijini Kengeja Kisiwani Pemba Wakiadhimisha Sikukuu ya Eid El Fitry Katika Viwanja vya Skuli Kengeja.

Tulioyarisi na kuyaacha bado yanaendelea kurisiwa,ndugu zangu nikiwa hapa jijiji kwetu Kengeja Kusini Pemba leo nimeshuhudia makundi ya watoto kutoka viunga tofauti vya hapa kijijini kwetu wakiendelea kifurahia sikukuu ya Eid.

Eneo hili tulitumia kaka zao siku kama hizi miaka ya nyuma ambapo sisi pia tulirisishwa na kaka na dada zetu leo wadogo zetu nao wanafurahia.

Kwa hakika haki inapendeza na inatua moyo kwa maana tulioyaacha yanaendelezwa.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.