Habari za Punde

Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa Azindua Wiki ya Mazingira Chuo Kikuu cha Ardhi (ARU) na Makampuni Lukuki Yashiriki Pia Maadhimisho Hayo.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla wakati alipowasili kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja kuzindua Maadhisho ya Wiki ya Mazingira, Mei 31, 2018. Wa nne (kushoto) ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, ambaye pia ana Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhandisi Evarest Ndikilo, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema na Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Dar es Salaam, Kate Kamba. (Picha na Robert Okanda Blogs)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo toka kwa Mkurugenzi Mtendaji Kampuni ya Space Engineering Philip Mtui aktika moja ya banda la nishati mbadala alipofanya uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya Mazingira, Mei 31, 2018 katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo. Kulia kwa Waziri Mkuu ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, ambaye pia ana kaimu Ukuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhandisi Evarest Ndikilo. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata Maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Edosama Hardware Limited, Edward Maduhu kuhusu bidhaa mbalimbali zinazotokana na miti ambazo zinatengenezwa na kampuni hiyo wakati alipotembelea mabanda ya maonyesho  kabla ya kuzindua Wiki ya Mazingira kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam Mei 31, 2018. Kushoto kwake ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba na Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Dar es Salaam, Kate Kamba (wa pili kushoto).
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Naibu Afisa Mtendaji Mkuu, wa Kampuni ya TMBM Powerspot Eco-Energy Limited, Lucas Singili namna wanavyoweza kutumia jiko la nishati mbadala kutengeza mwanga kwa matumizi ya nyumbani wakati Waziri mkuu aliptembelea bando la kampuni hiyo kabla ya kuzindua maadhiisho hayo. Kulia kwake ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kisare Matiku Makori.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Afisa Masoko wa Kampuni ya Falcon Packaging Anna Mrema jinsi wanavyotengeneza vifaa vya plastic ili kunusuru ukataji wa miti kwa kutengeza bidhaa hizo wakati alipotembelea banda lao katika maonyesho ya Wiki ya Mazingira kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam, Mei 31, 2018. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Chilambo General Trade Company, Gideon Chilambo wakati alipotembelea banda la kampuni hiyo kujionea bidhaa mbadala zinazotengenzwa kuzuia uharibifu wa mazingira. Waziri Mkuu alitembelea mabanda ya maonyesho  kabla ya kuzindua Wiki ya Mazingira kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam, Mei 31, 2018. Pamoja naye ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba (kulia kwake) na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, pia Kaimu Mkuu wa mkoa wa Mkoa wa Dar, Mhandisi Evarest Ndikilo (kushoto kwake).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Meneja Uendeshaji wa Kampuni ya AG Energies, Ibrahim Mussa wakati alipotembelea banda lao kujionea bidhaa mbadala zinazotengenezwa na kampuni hiyo kupunguza uharibifu wa mazingira. Wa tatu (kushoto) ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Pia Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhandisi, Evarest Ndikilo (kulia kwake)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza, Nimwagile Mwaijumba wakati alipotembelea banda lao na kujionea mashine za Kampuni ya Nyumbu ya kutengeneza mkaa bora kwa kutumia takataka iliyobuniwa na kutengenezwa na kampuni hiyo. Waziri Mkuu alitembelea mabanda ya maonyesho  kabla ya kuzindua Wiki ya Mazingira kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam, Mei 31, 2018. Wa tatu (kulia) ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Pia Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhandisi Evarest Ndikilo
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Mkurugenzi wa Kampuni ya JHS , David Mwendapole  wakati alipotoa maelezo kuhusu majiko makubwa yanayotumia  gesi kidogo  katika maonyesho ya Wiki ya Mazingira kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam, Mei 31, 2018. Wanne kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimia wananchi waliohudhuria uzinduzi wa maonesho hayo wakati alipozindua Wiki ya Mazingira kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam Mei 31, 2018. Kushoto (kwake) ni Waziri wa Mazingira na Muungano January Makamba na Meya wa Jiji la Dar es Salaam Yesaya Mwita.
Baadhi ya wananchi waliohudhuria katika maadhimisho ya wiki ya Mazingira wakimlaki Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipowahutubia kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, Mei 31, 2018. 
Baadhi ya wananchi waliohudhuria katika maadhimisho ya wiki ya Mazingira wakimlaki Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipowahutubia kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, Mei 31, 2018. 
Baadhi ya wananchi waliohudhuria katika maadhimisho ya wiki ya Mazingira wakimlaki Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipowahutubia kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, Mei 31, 2018. 
Baadhi ya wananchi na viongozi waliohudhuria katika maadhimisho ya wiki ya Mazingira wakimlaki Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipowahutubia kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, Mei 31, 2018. 
Mgeni Rasmi Mhe. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiiongoza meza kuu kuimba wimbo wa Taifa wakati alipowahutubia kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, Mei 31, 2018. 
Mkuu wa Idara ya Sayansi wa na Usimamizi wa Mazingira katika skuli ya Sayansi na mazingira wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU), Dkt. Chacha Nyangi akimpatia maelezo  mmoja wa wageni aliyetembelea banda la ARU, katika maonesho hayo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza jambo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba wakati wa kuagana na viongozi baada ya kuzindua Wiki ya Mazingira kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, Mei 30, 2018. Kutoka (kushoto) ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Pia Kaimu mkuu wa Mkoa wa Dar, Mhandisi Evarest Ndikilo, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamis Kigwangala, Mwenyekiti wa CC wa Mkoa wa Dar es Salaam, Kate Kamba, Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaviva. 
Sehemu ya wasanii wa Kikundi cha Dar Creators wakitoa burudani wakati wa uzinduzi wa maadhimisho hayo.
Afisa Msaidizi wa Afisa mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Trend Solar, Iman Ayoub akiwapatia vipeperushi na maelezo ya shughuli zifanywazo na kampuni hiyo walipotembelea banda lao kwenye uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya mazingira katika viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam Mei 31 2018.  
Msaidizi wa Mradi wa kuhamashisha matumizi ya Bioethanol kama nishati mbadala na safi kwa matumizi ya kupika, Alusaria nkya akifafanua jambo kwa wageni waliotembelea bandao la mradi huo, na maelezo ya jinsi ya kutumia nishati hiyo walipotembelea banda lao kwenye uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya mazingira katika viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam Mei 31 2018. Kushoto ni Afisa mwingine, Doroth Aminiel.
Mkuu wa Idara ya Sayansi wa na Usimamizi wa Mazingira katika skuli ya Sayansi na mazingira wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU), Dkt. Chacha Nyangi akimpatia maelezo  mmoja wa wageni aliyetembelea banda la ARU, katika maonesho hayo.
Mhadhiri Msaidizi wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU), Gervas Jonas  akitoa maelezo kwa sehemu ya wageni aliyetembelea banda la ARU, katika maonesho hayo.
 Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Pia Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhandisi Evarest Ndikilo (kushoto) akiagana na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamis Kigwangala baada ya kushiriki uzinduzi huo.

WIZARA, TAASISI ZA SERIKALI ZITUMIE NISHATI MBADALA – WAZIRI MKUU
*Aagiza viongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam wabadilike
*Ataka wasimamie wananchi waachane na matumizi ya mkaa
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameziagiza Wizara, mashirika na taasisi zote za Serikali na binafsi zianze kutumia nishati mbadala ili kuondoa kabisa matumizi ya kuni na mkaa.
Wizara, taasisi na mashirika yote ya Serikali na binafsi pamoja na vikundi vya uzalishaji wanaotumia nishati ya kuni na mkaa kwa ajili ya kupikia au shughuli za uzalishaji waanze kutumia nishati mbadala ili matumizi ya mkaa yaishe na ikiwezekana yatoweke kabisa,” amesema.
Ametoa agizo hilo leo (Alhamisi, Mei 31, 2018) wakati akizungumza na mamia ya wananchi na viongozi wa mkoa wa Dar es Salaam walioshiriki uzinduzi wa maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Kaulimbiu ya mwaka huu ni: “Mkaa ni Gharama: Tumia Nishati Mbadala.”
Waziri Mkuu amesema teknolojia bora ya uzalishaji wa mkaa mbadala ambayo ameiona kwenye maonesho hayo, ikuzwe na kusambazwa kote nchini ili kuwawezesha wananchi walio wengi waachane na matumizi ya mkaa wa kawaida na badala yake watumie mkaa-mbadala kwa lengo la kuhifadhi misitu na kupunguza uharibifu wa mazingira.
Ili kufanikisha matumizi ya teknolojia hiyo, Waziri Mkuu amesema vibali vya ujenzi wa majengo makubwa na taasisi kama shule, vyuo, hospitali navyo pia vianze kuzingatia ufungaji wa mifumo ya nishati ya gesi kwa ajili ya matumizi ya kupikia ili kurahisisha upatikanaji na matumizi ya nishati mbadala katika taasisi na majengo makubwa.
“Wahandisi na wachoraji ramani za majengo waweke njia za kupitisha kwenye michoro yao ili ujenzi wa nyumba na majengo haya ukikamilika, watumiaji waweze kutumia teknolojia hiyo,” amesema.
Wakati huohuo, Waziri Mkuu amesema Mkoa wa Dar es Salaam ni lazima ubadilike na uachane na matumizi ya mkaa. Kwa mujibu wa takwimu zilizopo, mkoa huo unatumia tani 500,000 za mkaa kwa mwaka.
“Viongozi wa mkoa na wilaya ondokeni hapa na hili kama ajenda ya mkoa wa Dar es Salaam, mkaifanyie kazi na Wizara pia ifuatilie mmetekeleza kwa kiasi gani. Jitihada zilizofanywa na Jiji la Dar es Salaam kupitia kwa Mstahiki Meya, za kuanza kuwapa mtaji wajasiriamali hawa wanaotengeneza teknolojia mpya ni lazima ziigwe na nyie kwenye Manispaa zenu.”
“Meya ametoa fursa na amewaanzishia, na ninyi sasa endeleeni. Tengenezeni bajeti kupitia Mabaraza ya Madiwani na muwaunge mkono wajasiriamali wanaotengeneza haya majiko kwa kuwapa teknolojia hii kwenye maeneo yenu. Wanaotengeneza mashine za mkaa mbadala, wawezeshwe watengeneze mashine nyingi zaidi na zije kila Manispaa, ili kila Manispaa ianze kutumia teknonolojia hiyo kupikia,” alisisitiza.
Amewaagiza Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Manispaa za Jiji la Dar es Salaam wafuatilie kwa karibu usambazaji wa teknolojia hiyo.
Kwa upande wake,

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.