Habari za Punde

Mchezo wa Ligi Kuu ya Zanzibar Nane Bora Kati ya Mafunzo na KVZ Uwanja wa Amaan Zanzibar Timu ya KVZ Imeshinda Bao 2-1.

 
Waamuzi na Wachezaji wa Timu ya KVZ na Mafunzo wakiingia Uwanja kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi Kuu ya Zanzibar Nane Bora.Mchezo uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar. Timu ya KVZ imeshinda mchezo huo kwa mabao 2-1. 
Mchezo huo kila timu imeonesha uchu wa kupata bao na kuoneshana mchezo wa kutegeana kila upande, katika dakika ya 35 ya kipindi cha kwanza mshambuliaji wa Timu ya KVZ ameiandikia bao la kwanza timu yake kwa shutu la mbali.

Nao wachezaji wa Timu ya Mafunzo wamejibu mashambulizi hayo katika dakika ya 39 mshambuliaji wa timu ya Mafunzo Ali Othman ameipatia bao timu yake la kusawazisha.Katika dakika ya 45 ya mchezo huo kipindi cha kwanza mshambuliaji wa Timu ya KVZ  Mohammed Masoud ameiandikia timu yake bao la pili na la kuongoza na kuibuka kidedea katika mchezo huo. 
Kikosi cha Timu ya Mafunzo kilichokubali kipigo cha bao 2-1 dhidi ya Timu ya KVZ, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Zanzibar Nane Bora mchezo uliofanyika katika Uwanja wa Amaan Zanzibar. 
 Kikosi cha Timu ya KVZ kilichoisambaratisha Timu ya Mafunzo kwa bao 2-1, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Zanzibar mchezo uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar. 
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.