Habari za Punde

WAZALISHAJI DAWA KUTOKA NCHI 25 WAKUTANA NA BOHARI YA DAWA (MSD) JIJINI DAR ES SALAAM

Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dkt. Mpoki Ulisubisya, akizungumza katika Mkutano ulioandaliwa na Bohari ya Dawa (MSD), uliowakutanisha  na wazalishaji wa dawa na vifaa tiba kutoka ndani na nje ya nchi uliofanyika leo Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam ambapo wazalishaji zaidi ya 
130 kutoka nchi 25 walihudhuria.
Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Rugambwa Bwanakunu akizungumza.
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Profesa Elisante ole Gabriel, akizungumza katika mkutano huo.
Viongozi mbalimbali wa MSD wakifuatilia  mkutano huo.
Wafanyakazi wa MSD wakiwa katika mkutano huo.
Wazalishaji dawa na vifaa tiba wakiwa kwenye mkutano.
Wafanyakazi wa MSD, wakiwa kwenye mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Mwakilishi wa Wazalishaji wa ndani, kutoka Kiwanda cha Prince Phermaceutical,Hetal Vitalan, akizungumza.
Kaimu Mkurugenzi wa Manunuzi wa MSD, Abdul Mwanja akizungumza.
 Kaimu Mkurugenzi wa Fedha na Mipango wa MSD, Sako Mwakalobo, akizungumza.
 Mkurugenzi wa Dawa na Bidhaa Nyongeza  wa  Mamlaka ya  Chakula na Dawa (TFDA), Adonis Bitegeko, akizungumza.
Wazalishaji dawa  wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali.

Na Dotto Mwaibale

KATIBU Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Dkt.Mpoki Ulisubisya, amesema uwezo wa Bohari ya Dawa (MSD), umeongeza na kupanua wigo wa uwekazaji na uzalishaji wa dawa nchini.

Akizungumza kwenye Mkutano wa pili wa mwaka wa MSD na wazalishaji na washitiri wa dawa na vifaa tiba zaidi ya 130 kutoka nchi 25, Dkt. Mpoki amesisitiza kuwa, MSD niya kiwango cha kimataifa hivyo milango iko wazi kwa wawekezaji wa dawa na vifaa tiba kuja kuwekeza nchini.

Aliongeza kuwa mkutano huo ni fursa ya kubadilishana uzoefu na kujadili namna yakufanya manunuzi,utekelezaji wamikataba na uimarishaji wa uwekezaji katika sekta ya afya.

“Tunaitikia wito wa serikali wa kuhakikisha wawekezaji wa ndani wanapewa kipaumbele, hivyo mkutano huu wakiutendaji,utaijengea uwezo MSD na kuongeza ushirikiano kati yake na wawekezaji wa viwanda vya dawa na vifaa tiba kwa kujua mahitaji aliyopo na kuwashauri soko tulilonalo ndani na njeya nchi ilikupanua wigo wautendaji,”alisema.

Aidha alisisitiza  kuwa  uwezo wa MSD katika usambazaji wa dawa na vifaa tiba umekua na  ndio sababu ya kukidhi viwango vya kimataifa, huku  mwaka wa fedha uliopita wakiwa wameweza  kutumia dola milioni 700 kwa ajili ya kufanya manunuzi.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Prof. Elisante Ole Gabriel, alisema utendaji wa MSD meboresha huduma za afya nchini na uhusiano wa karibu kati ya wizara yake na sekta ya afya nikichocheo muhimu cha uchumi nchini.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Rugambwa Bwanakunu, alisema hatua ya bohari kununua dawa moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji, imewawezesha kupanua wigo wa huduma na  kuwa karibu na wafanyabiashara na wawekezaji 160 alioingia nao mikataba, hivyo mkutano huo utawajengea uwezo na kuongeza ushindani kwa wazalishajihao.

Aidha, kwa upande wake mwakilishi wa wazalishaji wa ndani, kutoka kiwanda cha Prince Phermaceutical,HetalVitalan, lisema uimarishaji wa viwanda vya dawa na vifaa tiba  hapa nchini,umesaidia fedha inayotengwa na serikali katika bajeti ya dawa  kuweza kukuza uchumi wa ndani,kuongeza ajira kwa watanzania  na kupanua wigo waukusanyaji wa kodi kwa viwanda vya ndani.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.