Habari za Punde

Viongozi majimboni watakiwa kusikiliza na kutatua matatizo ya wananchi

Na Takdir Ali,       
   Viongozi wa Majimbo wamekumbushwa Wajibu kusikiliza na kutatua matatizo ya wananchi katika maeneo yao.
   Akizungumza na Wananchi na Viongozi wa Jimbo la Pangawe na Kijitoupele huko kwa Mabata Fuoni Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi ya Zanzibar            Abdallah Juma Sadala Mabodi amesema Wananchi wanawachanguwa Viongozi ili wawezen kuwasidia kutatua matatizo mbali mbali yanayowakabili.
   Amesema bado baadhi ya Wananchi Wanakabiliwa na matatizo kama vile ya Maji safi na salama, barabara na Vikundi vya Ushirika hivyo ni budi kwa Viongozi hao kuweza kuelekeza nguvu zao kwa Wananchi waliowachaguwa kwa ajili ya kuwatumikia.
    Amewataka Viongozi kufahamu kuwa wamechaguliwa kwa ajili ya kuwatumikia Wananchi hivyo ni vyema kuwatumikia bila kujali Itikali zao za Kisiasa, Dini wala Kabila na kufanya hivyo ni kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi.
     Amesema Sheha ni Msaidizi wa Raisi katika eneo lake kwa hivyo ni vyema wajuwe jisi ya kuweza kuilinda miondombini ya kimaendeleo katika maendeo yao na etakaeshindwa  atashindwa atachukuliwa hatua za Kisheria.
    Pia amewaagiza Masheha kulinda na kusimamia miondombinu inayojengwa na Serikali ili iweze kufikia malengo yaliokusudiwa ya kuwatatulia wananchi kero zinazowakabili hasa zkatika maeneo yaliodumu kwa muda mrefu.
    Mbali na hayo amewaomba Wananchi kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Viongozi wao na sio kuwavuja moyo kwa kuwapiga Majungu na Fitna miongoni mwao.
   Aidha ameipongeza Jumuiya ya Arika Muslim Ajens na Uongozi wa Jimbo la Pangawe kwa  kuwachimba  katika maeneo mbali mbali ya Jimbo hilo ambapo kwa kiasi kikubwa limeweza kuwatatulia tatizo la maji safi na salama katika jimbo hilo.\
    Mwakilishi wa Jimbo la Pangawe Mh. Khamisi Juma Mwalimu amesema kutokana na tatizo la maji safi na salama linalowakabili wananchi wameamua kulipa kipao mbele ili  jimbo hilo wameamua l uongozi wa Jimbo Umejipanga kwa hali na mali kuhakikisha wanawatatulia wananchi matatizo yao hatua kwa hatua.
   Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Pangawe Shamsi Vuai Nahodha amewataka Wananchi kushirikikiana na kuwa kitu kimoja katika kutatua matatizo yaliomo katika maeneo yao sambamba na kuepuka kufanya uharibifu wa miondombinu ya Maji na badala yake wawe mabalozi wazuri kwa wenzao.
      Zaidi ya Visima 9 vya Maji safi na salama vyenye gharama ya Sh. Milioni 11O vimechimwa katika maeneo mbali mbali ya Jimbo la Pangawe ikiwemo Fuoni meli 5, Kinuni, Pangawe, Muembemajogoo na Mnarani kwa lengo la kuwaepushia wananchi usumbufu wa kufuata huduma ya maji masafa ya mbali.   

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.