Habari za Punde

Waandishi wa Habari Wapata Mafunzo ya Kuripoti Habari za Udhalilishaji Kwa Kutumia Mitadao ya Kijamii Chini ya Mradi wa GBV Social Media na Udhalilishaji wa Jinsia.

Mratibu wa Miradi wa Taasisi ya TAMWA Zanzibar Bi. Asha Abdi akifungua mafunzo ya Siku Moja kuhusu Harakati za kutowa Elimu na Kuripoti habari za udhalilishaji wa Kijinsia kupitia Mitando ya Kijamii kupitia Mradi wa Social Media na GBV Udhalilishaji Jinsia, mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Tamwa Tunguu Zanzibar na kuwashirikisha waandishi wa habari wa Zanzibar. Mradi huo unasimamiwa na Tamwa Zanzibar.
Mratibu Miradi wa Taasisi ya Tamwa Zanzibar Bi. Asha Abdi akisisitiza jambo wakati wa kufungua mafunzo ya Siku moja kwa Waandishi wa Habari Zanzibar kuhusiana na Mradi wa Social Media na GBV, kuhusiana na vitendo vya Udhalilishaji wa Kijinsia. 
Afisa Rasilimali Watu wa Tamwa Zanzibar Bi. Tatu Ali akitowa Mada wakati wa Mafunzo hayo kwa Waandishi wa Habari Zanzibar kuhusiana na Mradi wa unaosimamiwa na Tamwa kuhusiana na kupiga vita vitendo vya Udhalilishaji wa Wanawake na Watoto Kijinsia unaojulikana Social Media na GBV, mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Tamwa Tunguu Zanzibar.No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.