Habari za Punde

Wakufunzi bora duniani: Guardiola, Zidane na Deschamps kushindania tuzo ya Kocha Bora wa Mwaka 2018

Zidane aliisaidia Real kushinda mechi 104 kupata sare mechi 29, na kujipatia asilimia 69.8% ya ushindi mbali na mataji tisa.
Aliyekuwa meneja wa Real Madrid Zinedine Zidane na kocha wa timu ya taifa ya Ufaransa aliyeshinda Kombe la Dunia Didier Deschamps ni miongoni mwa wakufunzi 11 walioorodheshwa kushindania tuzo ya Fifa ya Kocha Bora wa Mwaka 2018 duniani.
Kocha wa timu ya taifa ya England Gareth Southgate pia yuko kwenye orodha hiyo baada ya kuwaongoza kufika nusufainali Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza tangu 1990.
Meneja wa Manchester City Pep Guardiola, Jurgen Klopp wa Liverpool na kocha wa Ubelgiji Roberto Martinez wameorodheshwa pia.
Kocha wa timu ya kinadada ya Chelsea Emma Hayes yupo kwenye orodha ya makocha wa kike.
Chini ya Southgate, England walifikia kiwango cha juu zaidi walichowahi kufika wakicheza Kombe la Dunia wakiwa ugenini.
Guardiola naye alishinda Ligi ya Premia na kuweka rekodi ya kushinda mechi nyingi zaidi msimu mmoja ligi hiyo. City walikuwa klabu ya kwanza kufunga mabao 100 katika ligi kuu.

Gareth SouthgateHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionGareth Southgate aliwaongoza England kufika nusufainali Kombe la Dunia mara ya kwanza tangu 1990

Klopp aliwaongoza Liverpool kufika fainali Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya ambapo walishindwa na Real Madrid mwezi Mei, huku naye Martinez akiwasaidia Ubelgiji kuandikisha matokeo yao bora zaidi Kombe la Dunia kwa kumaliza wa tatu baada ya kuwashinda England. Ubelgiji walikuwa wamewatoa Brazil robofainali.

Ufaransa Euro 2016 na Kombe la Dunia 2018Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionUfaransa walishinda Kombe la Dunia miaka miwili baada ya kumaliza wa pili Euro 2016

Kocha wa Ufaransa Deschamps aliibuka wa tatu (baada ya Mario Zagallo na Franz Beckenbauer) kushinda Kombe la Dunia akiwa mchezaji na kocha pia.
Upigaji kuwa utafungwa saa sita usiku 10 Agosti, na sherehe ya kutoa tuzo itafanyika London mnamo 24 Septemba.
 • Massimiliano Allegri (Ita) - Juventus
 • Stanislav Cherchesov (Rus) - timu ya taifa ya Urusi
 • Zlatko Dalic (Cro) - timu ya taifa ya Croatia
 • Didier Deschamps (Fra) - timu ya taifa ya Ufaransa
 • Pep Guardiola (Spa) - Manchester City
 • Jurgen Klopp (Ger) - Liverpool
 • Roberto Martinez (Spa) - timu ya taifa ya Ubelgiji
 • Diego Simeone (Arg) - Atletico Madrid
 • Gareth Southgate (Eng) - timu ya taifa ya England
 • Ernesto Valverde (Spa) - Barcelona
 • Zinedine Zidane (Fra) - Real Madrid

Emma HayesHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionEmma Hayes aliwaongoza Chelsea Ladies kushinda ligi yanyumbani na kombe la ligi msimu uliopita

Hayes kushinda tuzo ya wanawake
Hayes, 41, aliwaongoza Chelsea Ladies kushinda Kombe la FA na Kombe la Ligi Kuu ya Wanawake siku chache kabla yake kujifungua mtoto mvulana.
Kwenye orodha hiyo yupo pia kocha wa zamani wa Chelsea Ladies Mark Parsons, ambaye sasa anaongoza Portland Thorns ya Marekani.
Orodha hiyo ya makocha wanne iliandaliwa na jopo la wataalamu wa Fifa ambalo lilimjumuisha nyota wa zamani wa Marekani Mia Hamm.
 • Emma Hayes (Eng) - Chelsea Ladies
 • Stephan Lerch (Ger) - VfL Wolfsburg
 • Mark Parsons (Eng) - Portland Thorns
 • Reynald Pedros (Fra) - Olympique Lyonnais
 • Alen Stajcic (Aus) - timu ya taifa ya Australia
 • Asako Takakura (Jpn) - timu ya taifa ya Japan
 • Vadao (Brz) - timu ya taifa ya Brazil
 • Jorge Vilda (Spa) - timu ya taifa ya Uhispania
 • Martina Voss-Tecklenburg (Ger) - timu ya taifa ya Uswizi
 • Sarina Wiegman (Ned) - timu ya taifa ya Uholanzi

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.